MBINU 30 ZA KUFANYA NDOA IWE
YENYE FURAHA NA AMANI
1. KUFAHAMIANA
/KUSOMANA VIZURI (Knowing self and knowing your partner)
Mhubiri 4:9-12
Afadhali wawili kuliko mmoja maana wapata ijara njema kwa kazi yao
Ebrania 13:4 Ndoa na iheshimiwe na watu wote na malazi
yawe safi
Kila mwanandoa anapaswa kujitambua kwanza
halafu atambue mambo mwenzi wake anayoyapenda na mambo asiyoyapenda
1. KUSHIRIKIANA,KUPATANA,KUKUBALIANA,KUGAWANA
(SHARING ,COOPERATION)
Wenzi wa ndoa
wanatakiwa kushirikiana katika mambo yote siyo kushindana (Cooperation not
competition)
Wanashirikiana
katika:
a)Mipango ya pamoja :
Bajeti
Matembezi
Aina ya uvaaji
Chakula –kula pamoja ,ratiba ya chakula ya pamoja
Vinywaji
Mapato na matumizi
Kulea watoto
Miradi
Biashara
Kazi
b)Kusaidia familia zao za pande zote mbili
c) Kufanya tathmini
ya maendeleo ya familia kiroho na kimwili
d)Kugawana kazi au kufanya kazi pamoja
e) Kuhudumiana katika mahitaji yote ya kiroho na kimwili
f) Kushirikiana maana yake ni kuacha ubinafsi wa aina
yoyote.
g) Kuchangia kila kitu : kabati,simu,begi,akiba….
3. KURUDI KWENYE
MSINGI WA NDOA (REVIVE YOUR MARRIAGE)Mithali 11:3
a) Kwa wale ambao hawajaoana kwa kufanya Harusi
·
waende kanisani wabarikishe ndoa yao
· wachumba wafunge ndoa (Wafuate kanuni za kiroho
na za kimwili) Mwanzo 2:21-24
b) Kwa wale walioowana kwa harusi
Wakumbuke
maagano waliofanya siku yao ya harusi mbele ya mashahidi wengi
1.
KUHESHIMIANA Mithali 11:16
Mke amheshimu mume na mume kadhalika amheshimu mke
Isiwepo dharau ya aina yoyote baina ya mke na mume bali
kila mmoja amheshimu mwenzi wake katika yote.Aheshimu mawazo yake,mapendekezo
yake ,mipango na maono yake ....
2. KUDUMISHA
UPENDO
Mithali 10:12, 1 Korintho 7:1-2
Mume ampende mke wake
na mke amtii mume wake.
Linda penzi
lisififie wala lisife
Mkumbushe mpenzi wako maneno yafuatayo “I Love you””Nakupenda” unapokuwa naye na ”I
miss you “anapokuwa hayupo.
Ili kudumisha
upendo fanya mambo 4 yafuatayo:
1)
2.Pokea upendo
1 korintho 7:3
2)
3.Toa upendo 1 korintho 7:4-5
3)
4.Tunza upendo 1 Korintho 7:10-11
3.
MTANGULIZE MUNGU KATIKA YOTE
MNAYOYAFANYA ,MCHENI MUNGU Mathayo 6:33
Mpe Mungu nafasi ya kwanza popote muwapo ,msikilize Mungu
na mumusikie kwa kifupi Ishini kwa imani.Utafuteni kwanza ufalme wa Mungu .
1. MTHAMINI
NA MTHAMINISHE MWENZI WAKO
Muone kwamba ndiye mzaliwa wako wa kwanza (First born)na
rafiki yako wa kwanza na wa kudumu.Mithali 17:17a
Mthaminishe katika kumsema vizuri ,kujitunza mwenyewe
.Kuwa kielelezo kwa watu wengine.nk...
2. RIDHIKA
NA MLIVYO NAVYO
Furahia hali mlionayo
, Hali ya :
ü
Uchumi
ü
Uzuri wa mwenza wako
ü
Elimu ya mwenza wako
ü
Mapungufu ya kiafya mlionayo wote
ü
Aina ya watoto
wenu(Albino,weusi,weupe,wembemba,wafupi,warefu sana , wagonjwa,wa aina moja …)
Msitamani vitu vya
wengine wala maisha ya wengine.Kumbuka kwamba maisha
hayawezi kwenda kama unavyotaka kwa asilimia mia(100%)
3. THIBITISHENI
UAMINIFU KATIKA NDOA
Jaribuni kuwa
waaminifu katika ndoa yenu msisalitiane.
Jaribuni kuwa wawazi
mmoja kwa mwingine kwa yote mnayoyapitia.Kumbuka kwamba malipo ni hapa hapa duniani ukiumiza
na wewe utaumizwa,ukidanganya na wewe utadanganywa,ukionea na wewe
utaonewa,ukisaliti na wewe utasalitiwa.Acha Michepuko baki njia kuu.
Uaminifu katika ndoa
ni nyuzo muhimu sana katika maendeleo ya ndoa hivyo ni vema kuulinda kwa
kujitunza.
4. SAMEHEANENI
Chukulianeni . Sameheaneni bila masharti .Epuka lawama 1
Tesalonika 5:23
Ondoa uchungu moyoni ,jipe amani.Kukosana kupo ila
inabidi msamaha uwekwe mbele.
Rekebisha na maliza matatizo mara baada ya kutokea
msichelewe chelewe.
Jaribu kusamehe na kusahau.Yaliyopita si ndwele ,ganga
yajayo.Msiyakumbuke yale yaliyojitokeza hapo nyuma maana yanaumiza moyo .Ipo
kanuni moja ya kibiblia inayosema kwamba ni lazima tusamehe saba mara sabini
,na nyingine inasema kwamba endapo hatutawasamehe wakosa wetu nasi Mungu naye
hatatusamehe makosa yetu.
5.
PONGEZANENI
KWA FURAHA
Mpeane hongera kwa :
ü
kufaulu mitihani
ü
kupata mtoto
ü
kupata kazi
ü
kuhubiri vizuri
ü
kukuheshimisha
ü
kukukubali
ü
kukupa mwili wake
ü
kuwa mume/mke mwema
Mpeane Pole kwa:
·
matatizo
·
magonjwa
·
ajali
·
kupoteza
·
kufeli mtihani au jambo linguine linaloweza
kujitokeza
Mpeane zawadi au
surprise ya hongera kwa:
ü
kufaulu au kufanya vizuri kwa jambo lolote
ü
kufanya vizuri jambo fulani nk…
6. HUDUMIANENI
KWA FURAHA
Kila mtu atimize
wajibu wake kwa mwenzake ili amtimizie haki zake.Huduma ya :
·
Mwili katika tendo la ndoa (usimnyime mwenzako 1
Korintho 7:4-5)
·
Mapambo
·
Chakula ,maji,mavazi,
ü Hudumia wageni ,onyesha ukarimu kwao Mithali
11:25
ü Hudumia watoto wenu katika mahitaji muhimu yote.
ü Saidianeni kazi
ü Huduma zote zizingatie usafi.Ebrania 13:4
7. MSIFIANE
KWA MAZURI YOTE
ü
Msifiane ila msishindane
ü
Kwa uzuri
ü
Kwa tabia njema
ü
Kwa kuheshimishana
ü
Kwa kazi njema mnazozifanya (kazi ya Mungu nay a
kawaida)
8. FANYENI
KAZI KWA BIDII
Kila mmoja wenu ajishughulishe 1
Tesalonika 3:10 4:11 mhubiri 4:9-10
ü
Thesalonike 3:8,11
ü
Jitume kufanya kazi kwa sana
ü Msaidiane kazi.
9.
LINDA SIRI YA NYUMBA
YENU
ü Usiropoke ropoke Mithali 10:19 katika maneno
mengi hapakosi kuwa na maovu.
ü Msionyeshane ujeuri wa aina yoyote ile
.Mithali 13:2
ü
Kama vile jeuri ya mali au elimu,umri
10. MSIFUATE
MKUMBO (BE YOURSEVES)
ü
Kwa kula ,kwa kuvaa, kwa kutumia yafanye yote kulingana na kipato chenu.
ü Msisikilize wala kufuata maneno ya watu wa nje
(ndugu ,jamaa na marafiki)
11. KUWENI
WABUNIFU
Ubunifu katika :
ü
Kuzalisha kipato
ü
Kumtumikia Mungu kwa kiwango
ü
Kufurahishana na kuridhishana
ü
Kulea watoto
12.
DHIBITINI NA ACHENI TABIA MBAYA ZINAZOMKERA MMOJA WENU
Msirudie,msirudie msirudie tabia yoyote mbaya
inayowadharaulisha na kuwatengenisha katika ndoa
yenu.mfano:Hasira,uchafu,uzinzi,ukali,kiburi cha uzima,wizi,uvivu....
Mtawaliwe na tunda la Roho Efeso 5:7
Kuwa
wapole,wavumilivu,wanyenyekevu,waelewa,wasikivu,watulivu .
Jifunzeni kutokana na makosa yenu.
13.
IOMBEENI NDOA KILA WAKATI 2 Timotheo 2:1 sala,dua,maombi na
shukrani
Ndoa ina vita vingi ,hivyo bila maombi inaweza ikavunjika
muda wote aidha mmoja anaweza akadanganyika au akingiliwa na Ibilisi shetani
ili awe chambo cha kuvuruga kila kitu .Maombi ni muhimu sana.Mume amuombee mke
na mke amuombee mume wake na wote waombee watoto wao.
14. KUWENI
NA MOYO WA SHUKRANI
Kila mmoja amshukuru
mwenza wake kwa kila mazuri kama vile:
ü
Kukusamehe
ü
Kukupa chakula
ü
Kukupa zawadi
ü
Kukupa kitu chochote
15. LINDA
IMANI YENU NA DHAMIRI NJEMA
Msiende kwa kwa waganga
Msikate tama mkarudi nyuma kiimani 1
Timotheo 1:19
16.
MUWE NA MOYO WA KIASI KATIKA
MAMBO YOTE
1 Timotheo 2:9 1 Timotheo 2:15 katika imani
,upendo,utakaso na moyo wa kiasi.
Kiasi katika :
o
Ongea yenu
o
Kazi ya Mungu
o
Tendo la ndoa
Kuwasiliana na watu wengine
o Kupiga
simu na matumizi yake
o Kutuma
sms
24.
MTENGE MUDA WA KUWA PAMOJA (SPEND TIME TOGETHER)
Semezana (stori) cheka pamoja cheza pamoja.Panga mipango
ya pamoja nk...
Kuwa pamoja kunaongeza viwango vya upendo wa wanaondoa
husika .
17. WEKEZA
Weka akiba kidogo kidogo
Uchumi ni jambo
muhimu sana katika maisha ya ndoa .Uchumi unapodorora ndiposa matatizo
yanadhihirika kwa sababu wakati mwingine hali ya kukosa mahitaji madogo
madogo nay a msingi inawafanya wachikane
haraka hata wanapojaribiwa nje wanakuwa tayari kushawishika .Wanakosa namna
nyingine ya kujikwamua .
Kuweka akiba kidogo
kidogo ni jambo la msingi sana katika maisha ya ndoa kwa sababu mambo mengi
yanakaa vizuri yenyewe wala hakuna msongo wa mawazo unaopata mwanya wa kuwavaa
wenzi.
18. TAFUTENI
USHAURI KWA WATU WENYE HEKIMA NA BUSARA
Maisha ya Ndoa ni
chuo kikuu kuliko vyuo vyote duniani kwa sababu wapo hata wasomi wakubwa ambao
unakuta ndoa zao zinawashinda pamoja na usomi wao.Ni vema wanandoa mkawa na
mshauri anayewajenga , kuwapa ushauri na kuwaelekeza nini cha kufanya kuboresha
na kudumisha ndoa yenu.Ni vizuri zaidi kila mwenzi akawa na mshauri wake
Mwanamke atafute mshauri mwanamke na mwanaume atafute mshauri mwanume.Mtafute
mtu mwenye mafanikio kwenye ndoa lakini pia anayemjua Mungu .
o
Jaribuni kuomba ushauri kwa wale Waliofanikiwa
kwenye ndoa, Viongozi wa kanisa na wenye hekima.
o
Fuata semina za ndoa
o
Kila mmoja wenu awe na
mshauri wake wa ndoa.
19. LEENI
NA FUNDISHA WATOTO (TRAIN CHILDREN) KWA KUSHIRIKIANA
Mithali 22:6 Mlee
mtoto naye hataiacha ,hata atakapokuwa mzee
Wajibu wa kulea
watoto ni wa kila mzazi hivyo mnatakiwa kushirikiana kuwalea watoto mlio nao na
wale mtakaowazaa .Jaribuni kuwaonyesha upendo wa dhati upendo wa wazazi.Kila
mzazi kwa nafasi yake achukue muda wa
kukaa na familia na kujaribu kuwapa watoto ushauri na kuwajenga kisaikolojia
20.
EPUKENI MADENI NA MSIPENDE
FEDHA Ebrania 13:5
Ndoa zilizo nyingi zinashindwa kukaa kwa amani na utulivu
kwa sababu ya madeni wanakuwa nayo.Wapo wale wanaingia katika mikopo na madeni
bila kushirikisha wenzi wao matokeo yake mdai anapokuja anamdai mwenzi
asiyekuwa na taarifa yoyote kuhusu deni hilo jambo linalokuwa chanzo cha ndoa
kuvurugika.Ni vizuri kama mwanandoa mmojawapo amechukua deni mahali popote
ajaribu kumfahamisha mwenzi wake ili yasitokee mambo ya ajabu baadaye.
Ni vizuri pia kushirikiana kuchukua deni kwa makubaliano
ya pande zote mbili .
21. TUMIENI
VIZURI KIPATO CHENU (SPEND WISELY)
Mapato yenu yasizidi
matumizi.Tumieni kulingana na kipat chenu ndipo mtakapofanikiwa.Msijilinganishe
au kushindana na familia zingine katika
·
kununua vyakula,mavazi ,
·
kusomesha watoto kwenye shule nzuri .
·
Kutoa sadaka .
22. WASILIANA
VIZURI :
·
Ongea kwa upole
·
Toa majibu mazuri si kwa
kufoka wala kukaripia.
·
Lugha laini
·
Kunena pamoja
·
Maamuzi mamoja
·
Malengo mamoja
·
Kunia mamoja
·
Pendekeza
·
Toa maoni
·
Fanya tathmini pamoja
29.NIENI MAMOJA
2 Korintho 13:11 Mtimilike ,....nieni mamoja
Rumi 12:16 Msinie yaliyo makuu
Wanandoa wanaponia mamoja wanakuwa na nafasi
nzuri sana ya kufika mbali katika malengo yao,mipango yao na hatimaye wanafikia
mafanikio na maendeleo makubwa kama walivyonia.
30.ZINGATIENI USAFI ebrania 13:4
Ndoa na iheshimiwe na watu wote na malazi yawe
safi.
ü Usafi wa mazingira ,
ü Usafi wa mwili
ü Usafi wa chakula
ü Usafi wa mavazi
ü Kutumia maji safi na salama
Ndoa nyingi zinavunjika kwa sababu ya wanandoa kutokuwa
wasafi.Mapenzi ni hisia za mtu .Kupenda au kutokupenda mtu kunatokana na hisia
za mtu mwingine anayehusika .Usafi kamili unapokuwepo ndoa haiwezi kupata doa
.Hata wageni wanapofika kwenye ndoa hiyo wanaisifia kwa usafi huo
walioushuhudia kwa macho yao. Kumbuka waswhili walisema kwamba Umaridadi
huficha umaskini .