Jumatatu, 29 Agosti 2016

KWA MSAADA WA MUNGU

KWA MSAADA WA MUNGU
            Matendo 26:22 Kwa kuwa nimeupata msaada utokao kwa Mungu
1.      Kwa msaada wa Mungu nitatenda mambo makuu.Zaburi 60:15  108:13
2.      Kwa msaada wa Mungu naruka ukuta  na kwa msaada wa Mungu nafuatia jeshi 2 Samweli 22:30 Zaburi 18:29
3.      Kwa msaada wa Mungu tutawapiga watesi wetu
4.      Kwa msaada wa Mungu nitalisifu Neno lake Zaburi 56:4,10
HEKIMA ANAONGEA maneno yafuatayo:
5.      Kwa msaada wangu wakuu hutawala na waungwana ,naam waamuzi wote wa dunia Mithali 8:16
6.      Kwa msaada wangu wafalme humiliki ,na wakuu wanahukumu haki Mithali 8:15

Hivyo basi :
7.      Kwa msaada wa Mungu:
o   Tutafanikiwa
o   Tutainuliwa
o   Tutafika mbali
o   Tutapanda viwango
o   Tutakubalika
o   Tutalindwa
o   Tutachanua

MANENO YA UKIRI WANGU

1.      Hakika wema na fadhili vitakaa nami siku zote za maisha yangu nami nitakaa nyumbani mwa Bwana daima zaburi 23:6
2.      Sitakufa bali nitaishi ili niyasimulie makuu ya Mungu
3.      Mimi ni mshindi zaidi ya kushinda
4.      Atakayenigusa atakuwa amegusa mboni ya jicho la Mungu


NA MWALIMU JAMES SADY

0717 820 980