Jumamosi, 24 Septemba 2016

NGUVU YA UAMINIFU


Uaminifu ni jambo la msingi na ni chombo  pekee kinachofaa ndani ya mahusiano mbalimbali, kama  ya biashara, mke na mume, mtu na mchumba,  marafiki na familia.uaminifu ni uwezo unaoleta imani kwa mtu, na ni njia  ya kukupeleka katika  ubora wako.
Si kila mtu anaweza kuaminika, tunatakiwa kuwa makini katika hilo, kwa sababu madhara yake ni makubwa sana. Imani inajengwa na historia ya mtu mmoja ambaye anaweza kuaminika na ni katika sehemu ambazo ameonekana kuwa ni mkweli na mwaminifu.
kitu kimoja cha ajabu sana kuhusiana na imani ni kwamba , inachukua miaka  kuijenga, lakini ni dakika kuibomoa.kuna namna nyingi ungeweza kumwamini mtu au la.  fuatana nami  katika maneno haya yanayoweza kuvutia, na kuamini neno moja inahitaji uvumilivu  mkubwa.
IMANI..INACHUKUA MIAKA KUIJENGA, SEKUNDE KUIBOMOA, NA HUTAWEZA KUITENGENEZA TENA.
1.         NI NINI?
·         Ni tunda la Roho Galatia 5:22
·         Ni kutenda kwa namna sahihi na watu sahihi ,mahali sahihi ukitumia vitu sahihi kwa wakati sahihi.
2.         FAIDA ZA KUWA MWAMINIFU Mathayo 25:21,23
·         Unaaminiwa na watu
·         Unahifadhiwa
·         Unakubalika
·         Unasaidiwa na watu
·         Unakopesheka
·         Macho yangu yatawaelekea waaminifu Zaburi 101:6

3.         UAMINIFU UNAJENGWAJE?
·         Kwa kuwa mkweli katika mambo yote
·         Kuishi maisha matakatifu
·         Usemi wako uendane na matendo

4.         JINSI YA KUISHI MAISHA YA UAMINIFU
·         Zaburi 89:8 unakuzunguka

5.         MADHARA YA KUTOKUWA MWAMINIFU
Mithali 25:19
·         Rushwa
·         Aibu
·         Uonevu
·         kudharauliwa

6.         VIWANGO VYA UAMINIFU Zaburi 119:138
·         Mwaminifu machache Mathayo 25:21-23

7.         KUTHIBITISHA UAMINIFU Zaburi 89:2
·         Kutenda kwa uaminifu 2 Nyakati 34:12  2  Falme 12:5  22:7
Yosea 2:14
Amuzi 9:16 
Zaburi 33:4
·         Kutenda uaminifu Mithali 12:22
8.         KUTOA KWA UAMINIFU
2 Nyakati 31:12

9.         ALAMA YA UAMINIFU YOELI 2:12

10.     KUMWITA MUNGU KWA UAMINIFU ZABURI 145 :18

11.     ROHO YA UAMINIFU MITHALI 11:13

12.     KAZI YA UAMINIFU

·         Huhifadhi Mithali 20:28
·         Ni mshipi wa kujifungia Isaya 11:5
13.     KUHUKUMU KWA UAMINIFU Mithali 29:14

14.     KUTAFUTA UAMINIFU  YEREMIA 5:1
·         Kupoteza uaminifu yeremia 7:28 Zaburi 12:1  waaminifu wametoweka.
·         Katika uaminifu yeremia 9:3
·         Kusema Neno kwa uaminifu yeremia 23:28
·         Shahidi wa uaminifu yeremia 42:5
·         Kuposa kwa uaminifu Hosea 2:20
·         Mtumwa mwaminifu mathayo 25:21
·         Kuonyesha Tito 2:10
15.     Kuwa mwaminifu katika
·         Utoaji
·         Utumishi
·         Muda
·         Usemi
·         Shughuli
·         Kimapenzi
·         Kibiashara
·         Kikazi
·         kirafiki
16.     Kuhesabiwa kuwa Mwaminifu Nehemia 13:13
17.     Ni mwamninfu katika nyumba yangu Hesabu 12:7
18.     Shahidi mwaminifu hatasema uongo Mithali 14:5
19.     Kuhani Mwaminifu 1 Samweli 2:35
20.     Nani mwaminifu kama Daudi 1 Samweli 22:14
21.     Mtu mwaminifu atakuwa na baraka Mithali 28:20
22.     Mji mwaminifu uwekuwaje kahaba Isaya 1:21
23.     Mji wa haki ,mji mwaminifu Isaya 1:26
24.     Mashahidi waaminifu Isaya 8:2
25.     Alikuwa mwaminifu hali kuonekana Daniel 6:4
26.     SIFA ZA MTU MWAMINIFU
·         Mjumbe mwaminifu mithali 15:13
·         Ni mwenye haki Isaya 1:26
·         Ni mtakatifu Hosea 11:12
·         Ni mkweli
·         Ni mwaminifu
·         Ni mwenye fadhili
·         Ni mwema
·         Ni mnyenyekevu

                                             MWALIMU JAMES SADY


SABABU ZINAZOWEZA KUSABABISHA MAOMBI YAKO YASIJIBIWE


Ndugu katika Krito , Bwana Yesu asifiwe,
Wakristo wengi wanaomba lakini hawapokei majibu ya mahitaji yao kutokana na kutokufahamu sababu mbalimbali zinzazoweza kuwa sababisho la Mungu kutokujibu maombi yao. Wengi wanachoka kuomba baada ya kuona wanacheleweshewa majibu ya mahitaji yao lakini wanasahau kwamba zipo kanuni wangepaswa kuzifuata ili kuweza kupata majibu ya mahitaji yao kirahisi.
Maandiko yanasema katika kitabu cha Mathayo 7:7 Ombeni nanyi mtapewa ,tafuteni nanyi mtaona ,bisheni nanyi mtafunguliwa” Maneno haya  hayafanyi kazi kwa kila mtu ili mradi tu ameomba bali yanafanya kazi kwa watu maalumu wanaofuata kanuni za kiungu na kutendea kazi Neno la Mungu.
Hao  wanaoomba na kupewa ni Wana wa Mungu walio katika zizi la Kondoo wa Mungu si wale walio nje ya zizi la Kondoo wa Mungu au sio wale wasiofuta kanuni ,miiko na sheria za kiroho.Si rahisi mzazi akamsikiliza motto mkaidi,asiye mtiifu kwake ,anayesufuata mambo yake binafsi kwa maana anakuwa tayari kama mwana mpotevu.Yampasa huyo mtoto kwanza arudi nyumbani kwa mzazi wake ndiposa Mzazi ataweza kumkaribisha kwa furaha ,kumhudumia na kumsaidia katika mahitaji yake yote ya kiroho na kimwili.Itakuwa rahisi kumsikiliza mtoto wake watakapokuwa wapo pamoja.  
Biblia inasema kwamba Maombi ya Mwenye dhambi ni kelele mbele za Mungu na hivyo kuna haja ya kuwa msafi kwanza kabla ya kuomba ili upate majibu ya mahitaji yako kirahisi .Hiyo itatokea mara baada ya kurudi nyumbani mwa Mungu,ukatubu dhambi zako na kuanza kufuata kanuni za Kimungu.
Tena maneno ya Mungu yanasema hivi  Isaya 43:26 “Unikumbushe na tuhojiane ,eleza mambo yako upate kupewa haki yako” kwa maana kwamba zipo haki za mwana wa Mungu na ili kuzipata haki hizo inampasa amkumbushe Mungu na wahojiane ili baada ya Mungu kujiridhisha na Halie yake ya kiroho na namna anavyomuomba ipasavyo basi na ampe haki zake .
Biblia pia inasema kwamba tumletee Mungu hoja zenye nguvu Isaya 41:21 “kwa maana kwamba endapo tutamuomba Mungu bila kutoa hoja zenye nguvu yaani zenye mashiko na zenye mantiki nzuri hatutoweza kupokea kile tunachokiomba
Mungu ni Mungu wa Kanuni ,kabla ya kumjibu muombaji lazima atataka kujiridhisha kutokana na kile anachokiomba kuangalia kama kinaendana na Kanuni za kimungu za kupokea Majibu ya mahitaji.
Kabla ya kujibu muombaji Mungu anaangalia mambo yafuatayo:
  1. Hali ya kiroho ya muombaji
·         Yaani ukoje katika hali yako ya uhusiano wako na Mungu?
·         Umejiandaje kupokea majibu ya mahitaji yako?
·         Ufahamu wako una uwezo kiasi wa kustahimili nguvu ya majibu ya mahitaji yako?
·         Je hoja yako ina nguvu mbele za Mungu?
·         Una mzigo kiasi gani ndani yako wa kazi ya Mungu?
  1. Namna anavyoomba
·         Unaombaje ?
·         Unaomba kwa kusudi/lengo gani ?
·         Kwa nini unaomba kitu hicho
·         Jambo unaloliombea linasaidia vipi kupanua ufalme wa Mungu?
·         Nia au msukumo wako wa kuomba kitu hicho  ni nini?
Hivyo basi tuna kila sababu ya kujipima katika kuzichunguza sababu zinazoweza kusabababisha tukakosa kupata majibu ya mahitaji yetu.
Kuna makundi makuu manne ya sababu zinazofanya maombi ya wanadamu yasijibiwe na Mungu:
·      Dhambi za kiroho (Spiritual sins) – Mashaka ,Unafiki, Kiburi,mambo ya upuuzi,mzaha,kejeli  etc
·      Ukosefu wa uhusiano (Poor relationships) - ,kutokusamehe,ushenzi,fidhuli, uovu, Hasira, ghadhabu,matengano.
·      Dhambi  - mambo yote yanayohusiana na kutenda uovu(1 Kor 6:9,10)
·      Kuomba vibaya  -kukosa msimamo,Kukata tamaa, kutokufunga,kutokutumi Jina la Yesu etc.
Sababu hizo ni pamoja na :
1.      Kutokuomba kwa Jina la Yesu  Kristo Yohana 2:17-26  14:13-14 (Marko 16:17-18).
2.      Kutokutubu dhambi au kutokuomba Msamaha Isaya 59:1-2
3.      Kuwa na mashaka na maneno uliyoyasema ulipokuwa unaomba  marko 11:23
4.      Hali ya Kusitasita moyoni au Kuwa na mashaka na Mungu Yakobo 1:5-8 
5.      Kutokuamini Yesu Kristo Yohana 16:26-27
6.      Kutokuomba Mungu Yakobo 4:2
7.      Kuomba kitu unachotaka kitumie kukidhi tamaa yako yaani kuomba vibaya Yakobo 4:3
·         Tunapaswa kuomba mambo yanayoendana na mapenzi ya Mungu au yanayoleta utukufu wa Mungu .
8.      Kukosa maneno ya Mungu ya kutosha ndani ya moyo Yohana 15:7
9.      Kutokuwa mtendaji wa Neno la Kristo au kutenda mabaya 1 Petro 3:12
10.  Kukosa kukesha 1 Petro 4:7
11.  Kuhukumiwa na moyo binafsi 1 Yohana 3:21-23
12.  Unafiki katika sala  Mathayo 6:5,6
·         Kuomba ili uonwe na watu
13.  Kupayuka-payuka katika sala Mathayo 6:7
14.  Kukosa umoja miongoni mwa viongozi wa kikristo ,kutokupatana Mathayo 18:19
15.  Kukosa kifungo cha roho Marko 9:29
16.  Kutokusamehe Marko 11:25-26
·         Kabla ya kuomba unatakiwa kusamehe waliokukosea kwanza.
17.  Kukosa subira na kukata tamaa Luka 18:1-8
18.  Kiburi  Luka 18:11-12
19.  Hasira /ghadhabu na majadiliano 1 Timotheo 2:8
20.  Mazungumzo mabaya   1 korintho 15:33
Zaburi 66:18 mawazo mabaya
21.  Kutokuamini Ahadi za Mungu (imani haba)
22.  Kuendeleza uovu 2 Timotheo 2:19
23.  Tamaa mbaya 2 Timotheo 2:22
24.  Ugomvi 2 Timotheo 2:23 1 Timotheo 3:3
25.  Kushiriki dhambi za wengine 1 Timotheo 5:22
26.  Kushindwa kutunza walio wako 1 Timotheo 5:8
27.  Kushindwa kuzuia nafsi 1 Timotheo 5:6
28.  Kujaa Lawama 1 Timotheo 5:7
29.  Kutokuomba sawasawa na mapenzi ya Mungu 1 Yohana 5:14-15
30.  Kutokaa ndani ya Yesu Yohana 15:7
31.  Kuwa na imani isiyo na matendo Yakobo 2:17
32.  Kutosikia kilio cha wahitaji Methali 21:13
33.  Kutoshukuru Mungu (shukrani)Filipi 4:4-12
34.  Kutokaa kwa amani na mke wako
1 PETRO 3:7 [‘Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili; na kumpa mke heshima, kama chombo kisicho na nguvu; na kama warithi pamoja wa neema ya uzima, kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe’].


MWALIMU JAMES SADY 0717 820 980

PALILIA IMANI YAKO



Inatakiwa niipalilie imani yangu kwa sababu imani yangu ndio msaada wa maisha yangu, vilevile Imani niliyo nayo nikiipalilia vizuri ndio itakayo nisaidia kupata utawala wa rohoni, na ndicho kinachotakiwa kwa mkristo anayemwamini Yesu Kristo.

ANGALIZO NO. 1 :
      • Majaribu yaliyonizunguka yataondoka kwangu kadri Imani     yangu inavyokua .

      • Namna ambavyo naweza kuipalilia Imani yangu ikawa na mizizi ambayo itanisaidia kukabiliana na changamoto yoyote ile ni kuruhusu moyo wangu uelimishwe na Neno la Mungu   ( Biblia ).  

       •Hii inasikitisha wakristo wengi hupuuzia kujifunza Neno la Mungu ( kusoma Biblia ) ndio maana shetani amepata uwezo wa kuwaweka waamini chini ya mgandamizo

      • Mgandamizo hauwezi kuruhusu imani ya mkristo kupokea Baraka zake kutoka kwenye uso wa Mungu, kwa sababu mgandamizo huyapofusha macho ya imani ya mkristo ,kwa hiyo ni vigumu mkristo kutambua kusudi la Mungu katika maisha yake.

       •( Macho ya imani yakipofuka mkristo ataishi chini ya utumwa wa dhambi  )

       •Mkristo aliyepofuka macho ya kiroho hawezi kuwa na ufahamu wa kutambua Baraka za Mungu zinakuja kwake kwa njia gani.

               -Jambo la kufahamu katika maisha yangu kama mwamini wakristo tuliookoka lazima tuwe makini sana tunaishi katika maisha yenye changamoto na vipingamizi vingi sana, ndio maana inatakiwa kuziendeleza roho zetu katika kumfahamu Mungu zaidi ili tupate wepesi wa kuyafikia maono yetu

       • Nisipo ruhusu roho yangu kuendelezwa na Neno la Mungu Imani yangu itapoteza ujasiri wa kukabiliana na utawala wa giza.
              - Mfano mzuri katika Biblia wa mkristo aliyepoteza utawala katika roho ( ujasiri ) ni wana wa Skewa.  Matendo ya Mitume;  19:13-16
       •Mkristo anayeishi chini ya mgandamizo ndani yake hana mamlaka yoyote ya kukabiliana na ufalme wa giza.

       •Mkristo anayeishi maisha ya dhambi maisha yake hukosa mpenyo, vilevile mwanga wa ki-Mungu Mstari wa 16,

       •Imani ya mkristo ikikosa ujasiri ni vigumu kuruhusu mpenyo wa  Baraka

       •Mkristo ambaye haishi maisha ya ukweli kila jambo mbele yake litampa utata.

       •Mwamini akiamua kuipalilia imani yake kupitia Neno la Mungu changamoto zitakazo jitokeza mbele yake hazitakuwa na nguvu.

        •Ili niweze kuvuka kila changamoto inayojitokeza mbele yangu inatakiwa niruhusu Neno la Mungu kuyaongoza maisha yangu. Yohana 5:5-9 
         •Mgandamizo ukiyakalia maisha ya mwamini, imani aliyonayo hupoteza mwelekeo yaani hata kile anachokijua anakisahau
         *(Mkristo anayeishi katika maisha ya mgandamizo kamwe hawezi kuishi maisha ya ukweli mpaka afunguliwe, na inafahamika wazi maisha ya ukweli ndio yanayo ruhusu Baraka za Mungu kuambatana na mtu. )*
          •Sauti ya Mungu ni Neno lake kwa maana zaidi ninaposoma Biblia najibishana na Yesu Kristo uso kwa uso.
          •Wakristo wa leo hawaamini kwamba Biblia ni hai katika maisha yao ndio maana kanisa la leo  halisisitizwi kabisa katika kusoma Biblia, ndio maana wakristo walio wengi wameweka tegemezi zaidi katika kuombewa kuliko kukaa chini na kujifunza neno la Mungu likampa maarifa ya kumtoa katika matatizo aliyonayo.

NIKIIPALILIA IMANI YANGU ITANIPA FAIDA ZIFUATAZO : 
A. Kutembea na Roho Mtakatifu
B. Kupata mamlaka ya Neno ( Uumbaji )
C. Nguvu ( Power )

UFAFANUZI WA VIPENGELE HAPO JUU:
A. Kutembea na Roho Mtakatifu.
     o Mkristo anayeishi maisha ya Imani ndiye mwenye uwezo wa kutembea na Roho Mtakatifu kwa sababu mwamini wa aina hiyo anakuwa anaishi sambamba na mapenzi ya Mungu.
     o Roho Mtakatifu anajifunua kwa mkristo mwenye kina cha Neno la Mungu.
     o Nikiwa Mkristo nisiyekuwa na kina cha Neno ninakuwa ni Mkristo kimwili lakini kiroho sio Mkristo.
     o Mwamini anayetambulikana kwamba ni Mkristo katika roho ni Yule ambaye maisha yake anayaendesha kama Neno la Mungu linavyosema hata kitabu cha Warumi kimesisitiza . WARUMI 8: 13- 16,  

ANGALIZO NO. 2
     o Mkristo mwamini akiishi kwa kufuata maumbile ya kibinadamu yaani mapenzi ya mwili hawezi kuungana na Baraka za Mungu, kwa sababu Mungu kuna kitu amesema katika kitabu cha Wakorinto.
      o 1 wakorinto 6 : 17  -( Lakini yeye aliyeungwa na Bwana ni roho moja naye ).
Nini maana ya kuungwa na Bwana kama inavyosema  1kor 6:17 ?
      • Maana ya kuungwa na Bwana ni kuyafanya maisha yangu yakae chini ya muongozo wa neno la Mungu maana yake Biblia.
Wakristo  waamini  tunapata nguvu ya Mungu kupitia Neno ( Biblia).
Neno la Mungu ndilo linalompa mkristo mwamini nguvu( uwezo ) wa kukabiliana na ufalme wa giza

( Mkristo atakaye mwuona  Mungu ni Yule atakayeweka mizizi katika Neno la Mungu).
Katika kufundishwa Neno la Mungu(Biblia ) ninapata faida ya upeo wa ufahamu wangu kuongezeka ,kwahiyo itanisaidia namna ya kuambatana na Baraka za Mungu.
Nguvu ya Mungu inajiumba kwa mkristo ambaye ameamua kuutia moyo wake ufahamu wa kufundishwa Neno la Mungu.
( Nikiwa kwenye uwepo wa Mungu nahitaji kuwa na uhalisia wa kile kinacho tamkwa ndipo nitafanikiwa).
Wakristo wengi wanaokuwa kwenye uwepo  wa Mungu wanapoteza uhalisia  wa kupokea Baraka zao kwasababu misingi ya imani yao imejijenga katika vinavyoonekana.
Biblia ni nguvu ya mkristo anayemwamini Yesu Kristo.
Mkristo anayesoma Neno la Mungu katika imani lile neno linakuwa hai kwake kwahiyo hata atakapo kutana na majaribu atapata wepesi wa kupenya kwasababu nyuma yake kuna nguvu ya Neno la Mungu.
Mkristo aliyelifanya Neno la Mungu kuwa sehemu ya maisha yake  akawa analisoma katika misingi ya kiimani akaliheshimu na kuliamini  hila  yoyote ya shetani haiwezi  kumsogelea kwasababu Neno la Mungu humfunua shetani na kumuacha uchi mbele ya  macho ya mkristo anayeliamini Neno la Mungu Waebrania 4:12.
Ninapolisoma Neno la Mungu moyoni mwangu ninajengeka katika  nguvu za kiroho,kwahiyo kila jambo nitakalolifanya  au nitakalolikusudia moyo wangu utanipa ishara kwamba ni sahihi au si sahihi.
Wakristo wengi wametumia nguvu  nyingi sana katika kujiharibu, tena sanasana jamii ya waaminio ,kuliko kutumia nguvu nyingi kujijenga katika imani.
Mkristo akifundishwa Neno akapata nguvu za rohoni shetani hawezi kupata nafasi ya kuingiza uvamizi.
Nguvu inakuja katika moyo wa mwamini kadri mwamini anavyoongeza juhudi ya kulisoma Neno la Mungu
Zaburi 119:11
Madhaifu yanaingia katika maisha ya wakristo ,kwasababu mioyo yao inakuwa tayari imepoteza nguvu ya Neno la Mungu.
Moyo wa mkristo ambao umepoteza nguvu ya neno  tabia za mwilini yaani za kimwili huanza kujidhihirisha.
Nikiona tabia Fulani ya kimwili inaambatana na mimi au inanisumbua sana inatakiwa niongeze juhudi katika kusoma  Biblia na kufundishwa Neno la Mungu hapo nitapata mpenyo wa ushindi.
Tabia yoyote iliyofungamana na maisha ya mtu isiyompendeza Mungu ili iweze kun’gooka inatakiwa roho ya mtu huyo ielimishwe na Neno la Mungu  kwelikweli  kwasababu tabia haina tofauti na roho chafu, ndio maana Biblia Zaburi  119:9 imetoa siri ya ushindi.
Njia ya kuyafanya maisha yangu ya wokovu yawe safi ni namna nitakavyokuwa na juhudi katika kujifunza Neno la Mungu , hii husaidia zaidi kuyafanya maisha ya  mwamini kuwa karibu na uwepo wa Mungu.
FAIDA YA NGUVU YA NENO:
Moyo wa mwamini  ukiimarika katika Neno la Mungu ndani mwake  huzaliwa imani yenye uwezo wa kuumba ,jambo hili lilimkuta Petro na Yohana wakielekea hekaluni .
Matendo ya Mitume 3:1-.
Katika Matendo ya Mitume 3:4. Kuna kipengele ambacho Petro alisema “ tutazame sisi”  alikuwa akidhihirisha wazi nguvu ya Neno la Mungu iliyojawa ndani mwake.
( Kupokea kwa mkristo anayemwamini Yesu Kristo kunaanzia katika Roho).
Hata kitendo cha kutokuliamini Neno la Mungu ni uzinzi tayari.
Maisha ya wokovu nilionao yatakuwa salama  kama nikiweka jitihada za kutosha za kufundishwa Neno la Mungu ,faida nitakayoipata katika hilo maisha yangu yatakuwa chini ya uwepo halisi wa Kimungu