Ijumaa, 2 Septemba 2016

NGUVU YA DAMU YA YESU KRISTO

DAMU YA YESU
Damu ya Yesu ni Damu ya Mungu aliyejifanya mwanadamu kwa ajili ya kuja kumkomboa mwanadamu katika dhambi .Kwa hiyo Damu yake ilifanya kazi ya kuondoa sauti ya shetani ndani ya damu ya mwanadamu iliyokuwa imechafuliwa na shetani na kurudisha sauti ya Mungu kama ilivyokuwa awali kabla ya Anguko la Adamu na Hawa pia  na kutengua maagano yote yaliyokuwa yamefanywa na wanadamu kwa njia ya  kutolea sadaka za kuteketezwa kwa miungu wakitumia damu za wanyama na kuwarudisha katika mstari  na hali ya kuwa na maagano mazuri na Mungu wa Ibrahimu ,Isaka na Yakobo kupitia hiyo Damu.
Damu ya Yesu ni Damu ya thamani kuliko damu ya mnyama au mwanadamu yoyote maana haina ila wala waa kama tunavyosoma katioka kitabu cha 1 Petro 1:19 Bali mlikombolewa kwa Damu ya thamani ,kama ya mwanakondoo asiye na ila na waa ,yaani Kristo

Kwa sababu ya Utakatifu wake Damu ya Yesu inanena mema kwa ajili ya maisha ya mwanadamu kwa ujumla wake maana inalenga kumkomboa mwanadamu kutoka katika gereza la dhambi na kuonewa na shetani.Damu hii inaneana mema kwa ajili ya Afya,Ndoa ,Shughuli ,Uzao,Huduma,Mipango na kila kitu kilicho chema cha mwanadamu ili aweze kufanikiwa bila usumbufu wowote wa ibilisi.
Damu ya Yesu ikikunenea mema hakuna awezaye kutengua
Ebrania 12:24 na Yesu mjumbe wa agano jipya,na damu ya kunyunyizwa,inaneyo mema kuliko ile ya habili
Yohana 19:34 na mara ikatoka Damu na maji
1 yohana 5: 8-9 kwa maana wako watatu washuhudiao (mbinguni,Baba na Neno ,na Roho Mtakatifu na watatu hawa ni umoja).Kisha wako watatu washuhudiao duniani Roho,na maji na Damu na watatu hawa kupatana kwa habari  moja.Tukiupokea ushuhuda wa wanadamu ,ushuhuda wa Mungu ni mkuu zaidi kwa maana ushuhuda wa Mungu ndio huu ,kwamba amemshuhudia Mwanawe.
Kwa hiyo tuanaona kwamba Damu ya  Yesu inashuhudia yanayotendeka duniani kwa maana kwamba yote tuyatendayo Damu ya Yesu inayaona na kutoa ripoti mbinguni kwa Baba.
KAZI YA DAMU YA YESU
1.      Inanena mema Ebrania 12:24/1 Petro 1:2
2.      Damu ya Agano Ebrania 9:20 1Korintho 11:25-29 kutoka 24:6-8(Musa),Mathayo 26:28/27:24
3.      Hutusafisha makosa 1 Yohana 1:7/ufunuo 19:13/ufunuo 5:9/Ebrania 9:24
4.      Tunapata ushindi Ufunuo 12:11
5.      Amani tunapata Kolosai 1:20
6.      Husafisha dhamiri zetu Ebrania 9:24
7.      Kuhesabiwa haki Rumi 5:9
8.      Upatanisho Rumi 3:25
9.      Ondoleo la dhambi Ebrania 9:22/Ufunuo 1:5
10.  Hututakasa sisi Ebrania 13:12
11.  Hutuleta karibu na Mungu Kolosai 1:20-21
12.  Hutupa ujasiri wa kuingia kwenye uwepo wa Mungu Ebrania 10:19-22
13.  Hutukamilisha machoni pa Mungu Ebrania 10:14
 MLINGANISHO BAINA YA DAMU YA MNYAMA, DAMU YA MWANADAMU NA DAMU YA YESU
DAMU YA  WANYAMA
DAMU YA MWANADAMU
DAMU YA YESU
Haina uhai wa Mungu
Ina uhai wa Mungu
Ina uhai wa Mungu
Mnyama anapokuwa mdogo damu yake haina mawaa lakini inapokuwa kubwa ina mawaa.

Ina mawaa

Ni safi ,Haina mawaa,ni Takatifu
Haiwezi kuondoa dhambi
Haiwezi kuondoa dhambi
Inaondoa na kutakasa dhambi
Inatengeneza  Agano na Ibilisi baada ya Ukombozi kwa Damu ya Yesu
Kwa njia ya kutolewa Kafara za watu  inatengeneza agano na Ibilisi .
Inatengeneza  Agano na Mungu
Shetani anaitumia kufanya maagano na wanadamu
Shetani huitumia kufanya maagano na wanadamu
Mungu wa Ibrahimu ,Isaka na Yakobo anaitumia kufanya maagano na wanadamu 
Hutuleta karibu na shetani iwapo tutaitumia kufanya maagano au kwa manuizo.
Hutuunganisha na wanadamu wengine katika tendo la Ndoa.
Hutuunganisha na ibilisi endapo tunatoa kafara za watu.
Hutuleta karibu na Mungu
ANGALISHO:
Ibada yoyote inayofanyika kwa kutumia damu tofauti na Damu ya Yesu na Jina tofauti na Jina la Yesu Kristo hiyo ni ibada ya miungu .
Kuanzia ujio wa Yesu Hakuna aina ya damu yoyote inayoweza kutumika kufanya agano na Mungu aliye hai.
AHADI KUHUSU DAMU:             
1.      Yoeli 3:21 nitaitakasa damu ambayo sijaitakasa
2.      Yohana 6:53-54
3.      Ezekiel 16:6-9
DALILI YA NAFSI ILIYOFUNGWA HAIJAKOMBOLEWA KUTOKANA NA MAAGANO YA DAMU

  1. Mtu hushindwa kujitawala(mtu anashindwa kuweka mambo ya nyumba yake vizuri)
  2. Mtu mwenye matatizo yanayojirudia-rudia(mf magonjwa,kupoteza fedha…)
  3. Hali ya kutokuendelea katika maisha
  4. Anaishi maisha ya kuanza –anza na kushindwa-shindwa
  5. Kutojiamlia mambo yako mwenyewe(akili yako imepumbazwa).Maisha ya kutegemea kuambiwa ambiwa.
  6. Dalili ya kutumia nyuvu nyingi lakini matokeo madogo(mwanzo4:11)(kulima,kazi,biashara)kuishi maisha ya kukata tamaa    naishuhudia mbingu na nchi(ardhi) hushirikiana kutambua (laana na Baraka ) ardhi na mbingu hushirikiana katika kutoa mvua,kuzalisha …..
  7. Kurithi matatizo ya wazazi ,ya ukoo Ezekiel 16:44 alivyo mama ndivyo alivyo binti yake,alivyo baba ndivyo alivyo mtoto wa kiume.
  8. Ndoto mbaya-mbaya
  9. Kukosa ulichostahili kuwa nacho
  10. Kudharauliwa na watu waliostahili kukuheshimu(zaburi 113:7)
  11. Kuishi katika uhitaji wa kukithiri(ufukara)
  12. Kuishi bila mafanikio kifedha (hagai 2:8)
  13. Utasa wa kibinadamu,wanyama,ardhi,biashara
  14. Kuishi bila kazi,shuguli yoyote,kuwa ombaomba
  15. Kuishi katika mikosi na balaa(hasara juu ya hasara)
  16. Kuishi katika dhambi isiyoisha inayokufadhehesha Methali 28:13

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni