Inatakiwa niipalilie imani yangu kwa sababu imani yangu ndio
msaada wa maisha yangu, vilevile Imani niliyo nayo nikiipalilia vizuri ndio
itakayo nisaidia kupata utawala wa rohoni, na ndicho kinachotakiwa kwa mkristo
anayemwamini Yesu Kristo.
ANGALIZO NO. 1 :
• Majaribu yaliyonizunguka
yataondoka kwangu kadri Imani yangu inavyokua
.
• Namna ambavyo naweza
kuipalilia Imani yangu ikawa na mizizi ambayo itanisaidia kukabiliana na
changamoto yoyote ile ni kuruhusu moyo wangu uelimishwe na Neno la Mungu ( Biblia ).
•Hii inasikitisha
wakristo wengi hupuuzia kujifunza Neno la Mungu ( kusoma Biblia ) ndio maana
shetani amepata uwezo wa kuwaweka waamini chini ya mgandamizo
• Mgandamizo hauwezi kuruhusu
imani ya mkristo kupokea Baraka zake kutoka kwenye uso wa Mungu, kwa sababu
mgandamizo huyapofusha macho ya imani ya mkristo ,kwa hiyo ni vigumu mkristo
kutambua kusudi la Mungu katika maisha yake.
•( Macho ya imani
yakipofuka mkristo ataishi chini ya utumwa wa dhambi )
•Mkristo aliyepofuka
macho ya kiroho hawezi kuwa na ufahamu wa kutambua Baraka za Mungu zinakuja
kwake kwa njia gani.
-Jambo
la kufahamu katika maisha yangu kama mwamini wakristo tuliookoka lazima tuwe
makini sana tunaishi katika maisha yenye changamoto na vipingamizi vingi sana,
ndio maana inatakiwa kuziendeleza roho zetu katika kumfahamu Mungu zaidi ili
tupate wepesi wa kuyafikia maono yetu
• Nisipo ruhusu roho
yangu kuendelezwa na Neno la Mungu Imani yangu itapoteza ujasiri wa kukabiliana
na utawala wa giza.
-
Mfano mzuri katika Biblia wa mkristo aliyepoteza utawala katika roho ( ujasiri
) ni wana wa Skewa. Matendo ya Mitume; 19:13-16
•Mkristo anayeishi chini
ya mgandamizo ndani yake hana mamlaka yoyote ya kukabiliana na ufalme wa giza.
•Mkristo anayeishi
maisha ya dhambi maisha yake hukosa mpenyo, vilevile mwanga wa ki-Mungu Mstari
wa 16,
•Imani ya mkristo
ikikosa ujasiri ni vigumu kuruhusu mpenyo wa Baraka
•Mkristo ambaye haishi
maisha ya ukweli kila jambo mbele yake litampa utata.
•Mwamini akiamua
kuipalilia imani yake kupitia Neno la Mungu changamoto zitakazo jitokeza mbele
yake hazitakuwa na nguvu.
•Ili niweze kuvuka
kila changamoto inayojitokeza mbele yangu inatakiwa niruhusu Neno la Mungu
kuyaongoza maisha yangu. Yohana 5:5-9
•Mgandamizo
ukiyakalia maisha ya mwamini, imani aliyonayo hupoteza mwelekeo yaani hata kile
anachokijua anakisahau
*(Mkristo
anayeishi katika maisha ya mgandamizo kamwe hawezi kuishi maisha ya ukweli
mpaka afunguliwe, na inafahamika wazi maisha ya ukweli ndio yanayo ruhusu
Baraka za Mungu kuambatana na mtu. )*
•Sauti
ya Mungu ni Neno lake kwa maana zaidi ninaposoma Biblia najibishana na Yesu
Kristo uso kwa uso.
•Wakristo
wa leo hawaamini kwamba Biblia ni hai katika maisha yao ndio maana kanisa la
leo halisisitizwi kabisa katika kusoma Biblia, ndio maana wakristo
walio wengi wameweka tegemezi zaidi katika kuombewa kuliko kukaa chini na kujifunza
neno la Mungu likampa maarifa ya kumtoa katika matatizo aliyonayo.
NIKIIPALILIA IMANI YANGU ITANIPA FAIDA ZIFUATAZO :
A. Kutembea na Roho Mtakatifu
B. Kupata mamlaka ya Neno ( Uumbaji )
C. Nguvu ( Power )
UFAFANUZI WA VIPENGELE HAPO JUU:
A. Kutembea na Roho Mtakatifu.
o Mkristo anayeishi maisha ya Imani
ndiye mwenye uwezo wa kutembea na Roho Mtakatifu kwa sababu mwamini wa aina
hiyo anakuwa anaishi sambamba na mapenzi ya Mungu.
o Roho Mtakatifu anajifunua kwa
mkristo mwenye kina cha Neno la Mungu.
o Nikiwa Mkristo nisiyekuwa na kina
cha Neno ninakuwa ni Mkristo kimwili lakini kiroho sio Mkristo.
o Mwamini anayetambulikana kwamba ni
Mkristo katika roho ni Yule ambaye maisha yake anayaendesha kama Neno la Mungu
linavyosema hata kitabu cha Warumi kimesisitiza . WARUMI 8: 13- 16,
ANGALIZO NO. 2
o Mkristo mwamini akiishi kwa
kufuata maumbile ya kibinadamu yaani mapenzi ya mwili hawezi kuungana na Baraka
za Mungu, kwa sababu Mungu kuna kitu amesema katika kitabu cha Wakorinto.
o 1 wakorinto 6 :
17 -( Lakini yeye aliyeungwa na Bwana ni roho moja naye ).
Nini maana ya kuungwa na Bwana kama inavyosema 1kor
6:17 ?
• Maana ya kuungwa na Bwana ni
kuyafanya maisha yangu yakae chini ya muongozo wa neno la Mungu maana yake
Biblia.
Wakristo waamini tunapata nguvu ya Mungu
kupitia Neno ( Biblia).
Neno la Mungu ndilo linalompa mkristo mwamini nguvu( uwezo ) wa
kukabiliana na ufalme wa giza
( Mkristo atakaye mwuona Mungu ni Yule atakayeweka
mizizi katika Neno la Mungu).
Katika kufundishwa Neno la Mungu(Biblia ) ninapata faida ya upeo
wa ufahamu wangu kuongezeka ,kwahiyo itanisaidia namna ya kuambatana na Baraka
za Mungu.
Nguvu ya Mungu inajiumba kwa mkristo ambaye ameamua kuutia
moyo wake ufahamu wa kufundishwa Neno la Mungu.
( Nikiwa kwenye uwepo wa Mungu nahitaji kuwa na uhalisia wa kile
kinacho tamkwa ndipo nitafanikiwa).
Wakristo wengi wanaokuwa kwenye uwepo wa Mungu
wanapoteza uhalisia wa kupokea Baraka zao kwasababu misingi ya imani
yao imejijenga katika vinavyoonekana.
Biblia ni nguvu ya mkristo anayemwamini Yesu Kristo.
Mkristo anayesoma Neno la Mungu katika imani lile neno linakuwa
hai kwake kwahiyo hata atakapo kutana na majaribu atapata wepesi wa kupenya
kwasababu nyuma yake kuna nguvu ya Neno la Mungu.
Mkristo aliyelifanya Neno la Mungu kuwa sehemu ya maisha
yake akawa analisoma katika misingi ya kiimani akaliheshimu na
kuliamini hila yoyote ya shetani
haiwezi kumsogelea kwasababu Neno la Mungu humfunua shetani na kumuacha
uchi mbele ya macho ya mkristo anayeliamini Neno la Mungu Waebrania
4:12.
Ninapolisoma Neno la Mungu moyoni mwangu ninajengeka
katika nguvu za kiroho,kwahiyo kila jambo
nitakalolifanya au nitakalolikusudia moyo wangu utanipa ishara
kwamba ni sahihi au si sahihi.
Wakristo wengi wametumia nguvu nyingi sana katika
kujiharibu, tena sanasana jamii ya waaminio ,kuliko kutumia nguvu nyingi
kujijenga katika imani.
Mkristo akifundishwa Neno akapata nguvu za rohoni shetani hawezi
kupata nafasi ya kuingiza uvamizi.
Nguvu inakuja katika moyo wa mwamini kadri mwamini anavyoongeza
juhudi ya kulisoma Neno la Mungu
Zaburi 119:11
Madhaifu yanaingia katika maisha ya wakristo ,kwasababu mioyo yao
inakuwa tayari imepoteza nguvu ya Neno la Mungu.
Moyo wa mkristo ambao umepoteza nguvu ya neno tabia za
mwilini yaani za kimwili huanza kujidhihirisha.
Nikiona tabia Fulani ya kimwili inaambatana na mimi au inanisumbua
sana inatakiwa niongeze juhudi katika kusoma Biblia na kufundishwa
Neno la Mungu hapo nitapata mpenyo wa ushindi.
Tabia yoyote iliyofungamana na maisha ya mtu isiyompendeza Mungu
ili iweze kun’gooka inatakiwa roho ya mtu huyo ielimishwe na Neno la
Mungu kwelikweli kwasababu tabia haina tofauti na roho
chafu, ndio maana Biblia Zaburi 119:9 imetoa siri
ya ushindi.
Njia ya kuyafanya maisha yangu ya wokovu yawe safi ni namna
nitakavyokuwa na juhudi katika kujifunza Neno la Mungu , hii husaidia zaidi
kuyafanya maisha ya mwamini kuwa karibu na uwepo wa Mungu.
FAIDA YA NGUVU YA NENO:
Moyo wa mwamini ukiimarika katika Neno la Mungu ndani
mwake huzaliwa imani yenye uwezo wa kuumba ,jambo hili lilimkuta
Petro na Yohana wakielekea hekaluni .
Matendo ya Mitume 3:1-.
Katika Matendo ya Mitume 3:4. Kuna kipengele ambacho Petro alisema
“ tutazame sisi” alikuwa akidhihirisha wazi nguvu ya Neno la Mungu
iliyojawa ndani mwake.
( Kupokea kwa mkristo anayemwamini Yesu Kristo kunaanzia katika
Roho).
Hata kitendo cha kutokuliamini Neno la Mungu ni uzinzi tayari.
Maisha ya wokovu nilionao yatakuwa salama kama nikiweka
jitihada za kutosha za kufundishwa Neno la Mungu ,faida nitakayoipata katika
hilo maisha yangu yatakuwa chini ya uwepo halisi wa Kimungu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni