Jumamosi, 24 Septemba 2016

UNAHITAJIKA (YOU ARE NEEDED )

SOMO: UNAHITAJIKA (YOU ARE NEEDED)

Mathayo 9:37-38 Mavuno ni mengi watendakazi ni wachache.
ISAYA 6:8 Nimtume Nani ?
Dunia hii imejaa mambo mengi  yanayohitaji watu wa Mungu kuyarekebisha .Baada ya anguko la Adamu na Hawa Mwanadamu alipoteza nafasi kubwa na Kumiliki ,kutawala na kutiisha kama alivyokuwa amepewa na Mungu awali.mamlaka hiyo ilichukuliwa na Ibilisi shetani baada ya kufaulu kumdanganya na kumtenga Adam na Mungu.Uhusiano wa Mungu na Adam ulikorofishwa ndiposa laana ilianza kumpata na kuishi maisha yenye majuto ,taabu na dhiki.
Mwana wa Mungu Yesu Kristo alipokuja alirejesha ile mamlaka ya Adam kupitia ukombozi kwa Damu yake na mamlaka hiyo alituachia sisi tuliozaliwa mara ya pili.
Hivyo wewe uliyezaliwa kwa Mara ya pili ,wewe ni mtu wa thamani sana ,UNAHITAJIKA katika dunia hii kufanya mambo kadha wa kadha katika kurejesha Ufalme wa Mungu hapa Duniani.Hali iko hivi:
Dunia imejaa watu :
a)    Wanaoangamizwa na shetani kwa kukosa maarifa  Hosea 4:6
b)   Wasiomjua Mungu wa kweli ni yupi , waliopotea kabisa
c)    Wenye kukata tamaa ya maisha  ,wasio na matumaini tena
d)   Waliovunjika mioyo
e)    Waliosetwa
f)     Wenye kujaa ujinga wa kila namna ,wamepandikizwa roho ya uasi
g)    Ndugu ,jamaa na marafiki wenye kufungwa kiroho na za kimwili
h)   Wenye kupagawa na nguvu za giza wanaohitaji msaada wa ukombozi
i)     Wenye kupotea dhambini na hawana mtu wa kuwapelekea Habari njema ya Wokovu
j)     Wanaoonewa na shetani na kukandamizwa kabisa ,hawafurukuti maana wamepofushwa akili zao na ibilisi shetani.
k)   Wamefungwa kihisia,kisaikolojia,kiakili,kiroho na kimwili.
l)     Wasiojua nini cha kufanya ili kuondokana na hali zao zenye kutisha na kuhuzunisha nk….
Hivyo ndugu yangu Tambua kwamba UNAHITAJIKA !
Mwana wa Mungu popote ulipo ,chochote unachokifanya ,fahamu kwamba wewe UNAHITAJIKA !
Hivyo usibweteke ,usilale ,usijisahau  ,okoa jahazi watu wanaangamia.
Kumbuka “una hazina kubwa sana ndani yako inayoweza kuzaa matunda makubwa mno “
a)    Una uwezo wa kulisha maelfu
b)   Una uwezo wa kumuondoa mtu kifungoni
c)    Una uwezo wa kupindua mipango na hila za ibilisi
d)   Ukisimama kwenye zamu yako una uwezo kwa kufanya mambo yasiyo ya kawaida wakati ungali unaishi katika hali ya kawaida .Ndiyo maana Yesu anasema Ishara hizi zitamambatana na hao waaminio  ,Amwaminiye atatenda zaidi ya yale ambayo hakutenda.
Unahitajika
ü  kufanya kitu hapa dunani kwa ajili ya Bwana
ü  kusaidia hao watu waliotajwa hapo juu kubadili hali ya mambo
Mungu amekupa elimu uliyo nayo kwa makusudi .Elimu yoyote njema uliyo nayo (ya kiroho au ya kimwili) ,Mungu amewekeza ndani yako akitarajia kuwa na wewe utaitumia kusaidia wanaoihitaji na kwamba utaimbaza kwa wengine.
Hata Wazazi wamekusomesha wakitegemea kuja kusaidiwa na wewe baadaye.Unahitajika kuwarejeshea matumaini mazuri siyo mambo ya kuhuzunisha au kusikitisha .
Una hazina kubwa inayoweza kumsaidia jirani aliye karibu na wewe na aliye mbali.Ndiyo maana Yesu anasema Umpende Jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe maana yake umhudumie kadiri uwezavyo ukitumia hazina uliopewa kam tunu ya mabadiliko ya aina yoyote.
Maisha unayoishi yamefichwa ndani ya pakeji inayoitwa kusudi.Mhubiri 3:1 “ kwa kila jambo kuna wakati wake na kusudi chini ya jua “
Komboa wakati ili utimize kusudi.Galatia 5:16
Uliumbwa kwa kusudi maalum ndiyo maana hufanani na mtu yeyote duniani .Umewekewa na Mungu hazina kubwa ndani yako ili uweze kuitumia kutimiza kusudi hilo .hazina hiyo ndiyo inayokurahishia kutimiza kusudi la Mungu la kukuumba.KILE ULICHO NACHO ,KUNA MTU ANAKILILIA MAANA ANAKIHITAJI HAKIKA NA WEWE UNAHITAJIKA KUMRAHISHIA KUKIPATA APATE KUPONA.
Katika dunia hii ,Mtu wa Mungu anahitajika katika maeneo makuu mawili :
a)    Mambo ya kiroho
b)   Mambo ya kimwili
  1. KIROHO UNAHITAJIKA :
1)                 KUMTUMIKIA MUNGU (TO SERVE GOD ) :
         Unahitajika kutumwa na Mungu yaani kumtumikia ISAYA 6:8 Nimtume Nani?
         Mathayo 9:37-38 /Luka 10:2 Mavuno ni mengi watendakazi ni wachache.
                       Mifano ya watu waliohitajika wakafanya :
ü Yesu alihitajika kuja kukomboa wanadamu Yohana 3:16
ü Yusufu alihitajika kukomboa familia yake
ü Ibrahimu alihitajika kuwa Baba wa Imani wa Vizazi vyote
ü Nuhu alihitajika kubeba kusudi na mpango wa Mungu
ü Esther alihitajika kukomboa ukoo wake
ü Paulo alihitajika kupeleka injili kwa wasiotahiriwa
ü Petro alihitajika kupeleka injili kwa waliotahiriwa
Kila mtumishi wa Mungu kwenye Biblia (Nabii,Wafalme ,Mitume…) alihitajika kufanya kazi maalum  la kumtumikia Mungu aliyoitiwa kufanya  (Musa ,Yoshua walihitajika kuongoza wana wa Israeli Kanani  )Hivyo na wewe unahitajika kutimiza WITO wako kwa kumtumikia Mungu . Fanya kazi ya Bwana .
2)     KULETA MABADILIKO YA KIROHO KATIKA JAMII
a)    Kutia moyo waliovunjika Isaya 35:3-4 Itieni nguvu mioyo iliyo dhaifu
b)   Kupoza wagonjwa ,kufufua wafu,kutakasa ukoma Mathayo 10:8
3)     KUHUBIRI
a)    Kuhubiri injili yaani kumtangaza Kristo ( Habari njema ) duniani kote Marko 1:14
Mathayo 28:19-20 Basi ,Enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi ,mkiwabatiza kwa jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu .
                      Uwe tayari kwenda !  Marko 3:14
b)   Kueneza ufalme wa Mungu
4)     Kuombea kanisa , watumishi na watu wote 1 Timotheo 2:1
5)     Kutengeneza njia ya Bwana na Kunyosha mapito ya Bwana Mathayo 3:3
6)     Kusimama mahali palipobomoka
7)     Kuwa kielelezo katika usemi ,mwenendo ,upendo imani,usafi 1 Timotheo 4:12
8)     Kutumia karama iliyopo ndani yako 1 Timotheo 4:14
9)     Kuondoka  na kuangaza Isaya 60:1
10)  Kuamka usingizini Efeso 5:14    1 Tesalonike 5:6
11)  Kupiga vita vizuri vya imani 1 Timotheo 6:12
12)  Kuomba bila kukoma 1 Tesalonike 5:17
13)  Kuagiza na kufundisha 1 Timotheo 4:11
14)  Kufuata haki ,utauwa,imani,upendo,saburi na upole 1 Timotheo 6:11
15)  Kuenenda kwa roho Galatia 5:16
16)  Kusimama imara katika Bwana Filipi 4:1
17)  Kubadilika na kubadili hali ya mambo  kwa kujitenga na ubaya wa kila namna        
1 Tesalonike 5:22
18)  Kusimama kwenye zamu yako Habakuki 2:1
  1. KIMWILI UNAHITAJIKA :
  1. Kujenga mitazamo ya watu (People’s Mindsets transformation)
  2. Kusaidia wahitaji yaani kutenda mema 1 Tesalonike 3:13
Yatima ,wajane ,wagane ,wasiyojiweza,walemavu  
  1. Kuleta MABADILIKO ya kimwili popote ulipo
·         Mabadiliko ya kifra : Kubadili fikra na mitazamo ya watu kupitia kuwaelimisha
·         Mabadiliko ya kiuchumi
  1. Kuleta MAENDELEO kanisani ,kwenye family na katika taifa lako
  2. Kusaidia familia jamii ,marafiki na ndugu
·         Kiuchumi
·         Kimaendeleo
·         Kiafya
·         Kiakili
·         kielimu
  1. Kutunza walio wa nyumbani mwako 1 Timotheo 5:8
  2. Kujenga uchumi wa nchi , kwa kufanya kwa moyo kila jambo Mhubiri 9:10 Kolosai 3:23
  3. Kufanya kazi kwa bidii 1 Tesalonike 3:10-11  2 Tesalonike 4:11   2 Tesalonike 3:8
Chukua hatua sasa !
Mungu akubariki sana  !

MWALIMU JAMES SADY 0717 820 8980 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni