Ijumaa, 2 Septemba 2016

ONDOKA HAPO ULIPO

ONDOKA HAPO ULIPO 
   
ONDOKA UPESI HAPO ULIPO
Matendo ya Mitume 12: 1-19, zingatia sana mstari wa 7 unaosema; "...Ondoka upesi, Minyororo yake ikamwanguka mikononi"
ISAYA 60:1
"Ondoka uangaze; kwa kuwa nuru yako imekuja,
Na utukufu wa Bwana umekuzukia."
Anaposema, ONDOKA anamaanisha Utoke hapo ulipo pia Uinuke kutoka hapo ulipo maana ni mahali pa mateso yako, mahali pa huzuni yako na ni mahali palipokuchelewesha sana hivyo:
- Ondoka kwenye kuumwa umwa na uangaze ukiwa na uzima ndani yako.
- Ondoka kwenye kujikataa maana kulisababisha ukataliwe lakini leo ondoka hapo na Mataifa yatakujilia maana NURU YA BWANA IPO JUU YAKO (ISAYA 60:3)
*Magonjwa
* Umasikini
* kufeli
* kushindwa hakupo tena juu yako maana hiki ni kipindi chako cha KUINUKA NA KUANGAZA MWANA WA MUNGU.
ONDOKA KATIKA TABIA ZA KWANZA
Isaya 60:1-2 "Ondoka, uangaze; kwa kuwa nuru yako imekuja, Na utukufu wa Bwana umekuzukia.Maana, tazama, giza litaifunika dunia, Na giza kuu litazifunika kabila za watu; Bali Bwana atakuzukia wewe, Na utukufu wake utaonekana juu yako."
Ukiokoka jambo la kwanza amua kubadilika na uamuzi wa kubadilika unao wewe mwenyewe. Mtu akikuangalia akilinganisha maisha yako kabla ya kuokoka na baada ya kuokoka aone umebadilika. Katika kuondoka ndipo tunakutana na Utukufu wa Mungu, lakini ukiwa katika tabia za kwanza hutaona Utukufu wa Mungu.                          Utasikia wengine wakisimulia matendo ya MUNGU lakini kwako hutayaona.
Hapo kwanza ulikuwa mtu wa kawaida lakini leo kuna watu wakipata shida wanakutafuta ni kwasababu umeamua kuondoka.
Ukiona watu wanakusifia kwa mambo ya jana inamaana huna jipya leo, wokovu wetu ni sasa siyo jana, usijivune kwa jambo la jana bali jivune kwa jambo zuri unalofanya leo. Ni vizuri kuishi kwa tahadhari ili NURU yako isitiwe giza.

Tunatakiwa tusiishi kama watu wasio na matumaini bali tuishi kama wasafiri, wakati wote wana wa MUNGU tunatakiwa kuwa na muda wa ziada wa kujiandaa kwa safari.
Ugomvi wetu na MUNGU uko kwenye tabia zetu, hazitaki kubadilika na kuhama katika tabia za kale, lakini kuanzia leo hatutazikumbuka tena tabia za kale na tukizikumbuka ni ili kutubu na kutorudia tena. Mungu hajakuokoa ili ukae kanisani uonekane ni Mkristo hapana, amekuokoa kwa kusudi na mpango wake. Jichunguze ulipo ni sawa na hilo kusudi?
Ukiona mwenzako amefanikiwa na kuchanua, MUNGU anambariki au anafanya vizuri katika utumishi wake na wewe unamzuia au roho inaumia ujue wewe na pepo hamna tofauti maana unapingana na MUNGU, ukijua wewe ni mtu wa aina hiyo rudi umwambie MUNGU sitaki kuwa kama pepo nisamehe na unibadilishe.
Wana wa mungu ukiona mwenzako amefanikiwa nenda kamuulize, mwenzangu unatumia mbinu gani? Sio unaanza kumwekea kinyongo. Haupo ili kumsaidie shetani bali unatakiwa kumsaidia MUNGU maana sisi ni MIUNGU.



1.   Mungu alimwambia Ibrahimu atoke katika Nchi ya baba yake

2.   Lutu  na jamaa yake walikaa Kanaani pamoja na Ibrahimu na baada ya muda waliachana wakagawana ardhi Lutu akachagua Wilaya ya Yordani akahamia huko na jamaa yake na wanyama hatimaye wakakaa katika mji wa sodoma ..watu wa sodoma walikuwa wabaya sana ,Lutu alisumbuliwa maana alikuwa mtu mzuri.Hata Mungu alisumbuliwa. Mwishowe Mungu alituma malaika wawili wakamwonye lutu kwamba Mungu ataharibu sodoma na gomora mji wa karibu maana ni miji mibaya.malaika wakamwendea Lutu wakamwambia “Fanya haraka ,chukua mke wako na binti zako wawili MWONDOKE huku! Malaika mmoja alisema “Kimbieni kwenye milima msiuawe”Lutu na binti zake WAKATOKA sodoma lakini mke wa Lutu hakutii .walipokwisha kutembea mwendo Fulani kutoka sodoma ,mke alisimama akatazama nyuma akawa nguzo ya chumvi.
             Mwa 13:5-13 18:20-33 19:1-29 Luka 17 :28-32 2 Petro 2:6-8 
3.   Yohana 5:7 Sina mtu wa kunitia birikani
             Luka  5: 24-26 Ondoka ,jitwike  kitanda chako,ukaende zako nyumbani kwako.
           Yohana 11:39 liondoeni jiwe.
          Mathayo 23: 35 Mwanamke aliyetokwa na damu. Mwanamke huyu aliondoka kwenye taabu yake (Magonjwa )
USHAURI
o   Usifurahie kukaa mahali ulipo kwa muda mrefu  maana siyo mpango wa Mungu udumae usitoke hapo ulipo
o   Kamwe usiridhike na hali uliyonayo .
o   Lazima cheo chako na hadhi yao viendane.
Kazini Mungu anahitaji upande viwango
Katika huduma Mungu anapenda huduma yako iongezeke zaidi
Katika biashara Mungu anahitaji uongeze mtaji na upate maendeleo ya ziada

Mungu :
o   Ni Mungu wa maendeleo
o   Ni Mungu wa mazao
o   Ni Mungu wa maongezeko
o   Ni Mungu Mtawala
o   Ni Mungu wa viwango
o   Ni Mungu wa mabadiliko
o   Ni Mungu wa tofauti
Mungu anatumia alama ya :
a)   kujumlisha (+) na
b)   kuzidisha (X)
c)   kugawa ( : ) Luka 5:7
Aliye na joho mbili ampe na mwingine Mathayo 10 :

Hali kadhalika anatutaka na sisi pia tuwe kama yeye alivyo .
o   TUENDELEE
o   TUZAE  (Anataka tumzalie matunda ya kiroho na ya kimwili)Mwanzo 1:28
o   TUONGEZEKE (anataka tuongezeke katika maeneo yote ya maisha yetu) Mwanzo 1:28
o   TUIJAZE NCHI Mwanzo 1:28
o   TUTAWALE tusitawaliwe
o   TUWE NA VIWANGO
o   TUBADILIKE
o   TUWE WA TOFAUTI
Mpango wa Shetani ni kutaka sisi tukwame ,tusisonge mbele ,tudumae tusiendelee wala kupata mafanikio hata kidogo . Kazi yake ni kuiba ,kuharibu na kubomoa Yohana 10:10
Mungu anataka tutoke/ katika :
Aina za mikwamo:
a)   Mkwamo wa kimwili
b)   Mkwamo wa kiroho

MKWAMO WA KIROHO
1)   Imani haba na potovu( Uchanga wa kiroho )
2)   Tabia mbaya
3)   Upofu  wa kiroho (bartimayo)
Efeso 1:6 Macho ya mioyo yatiwe  nuru mpate kujua kusudi la Mwito wenu katika Kristo Yesu.

MKWAMO KIMWILI
1)   Magonjwa
2)   Ufukara
3)   Ujinga

Hatua za kuondoka mahali ulipo:
1.   KWANZA UNAINUKA
2.   PILI UNASIMAMA
3.   TATU UNAONDOKA

A) INUKA
Isaya 62:1 Inuka uangaze maana nuru yako imekuja.
 …………..Inueni vichwa vyenu enyi malango
Huku kuinuka kunatokana na maamuzi uliyonayo ya kuchoka hali uliyonayo kwanza na ukaamua kuiacha
Kuinuka ni kufanya mkaguo wa maisha yako ,unafanya tathmini ya maisha yako
Kuinuka ni kugundua tatizo na kusudi la kuumbwa kwako.
Mifano :
a)   Mwana mpotevu akawaza moyoni mwake .
b)   Mwanamke aliyekuwa anatoka damu.


KIU ,TAMAA,SHAUKU
Kabla ya kuinuka unahitaji kwanza shauku ,hamu ,kiu (desire )ya kuwa vile unavyotaka kuwa .
“Huwezi kuwa usivyotamani kuwa”
Ila waweza kutamani. Kutamani kuwa katika viwango vingine vya utumishi na imani

KUFUNGWA KWA AKILI
o   Watoto waliozaliwa kwenye mlima wakakulia huko huko walipopelekwa barabarani na mjini walishindwa kuelewa.
o   Wengine wamefungwa na mila zao na tamaduni.(uchawi ,ulozi)
o   Wengine wana maono ya kanisa moja tu mapokeo ya kanisa na itikadi za dini yake.
o   Wengine wana maono ya mkoa moja au wilaya .
o   Wengine wanaona familia zao tu hawajali jamii  Biblia inasema “Enendeni ulimwenguni mwote”

KUNA WATU WAMERIDHIKA NA HALI ZAO HAWATAKI KUONDOKA WALIPO
a)   Mlemavu moja alikuwa ombaomba ,alizoea upata hella nyingi.siku moja akaja mtumishi wa Mungu kumuombea uponyaji asiwe mlemavu yeye akakataa kwamba hawezi kukubali kuombewa kwa sababu anaogopa atakavyoishi baadaye.

VITU VINAVYOINUA MTU
b)   Kuishi maisha ya maombi
c)   Kuthubutu :kuchukua hatua ya kuanza kitu Fulani la Maendeleo
o   Mwanamke aliyekuwa birikani alishindwa kuthubutu kujaribu kuingia birikani.
d)   Kuanza mawazo ya biashara na kuiendeleza
Mtu anaweza kuajiriwa mahali lakini anazidi kulalamikia bosi badala ya kuchukua hatua ya kutafuta kazi sehemu nyingine.

B) SIMAMA
Isaya 3:13 Bwana asimama ili atete
Isaya 40:8  Shauri langu litasimama
Kusimama ni tabia  ya Mungu  maana halali wala hasinzii .
ü  Nahumu 2:8  Simameni ,simameni ,simameni.
ü  Mika 6:1 Simama ujitetee.
ü  Mika 7:8 Niangukapo nitasimama tena.
ü  Habakuki 2:1 Nitasimama katika zamu yangu
ü  Efeso 6:13 Simameni hali mmejifunga kweli viunoni
ü  Yohana 8:44 Simama katika kweli
ü  Ezekiel 2:1 Mwanadamu simama kwa miguu
ü  Ezekiel 22:30 Simama mahali palipobomoka
ü  Yeremia 46:4 Simameni na chapeo zenu
ü  Yeremia 51:50 Msimame mkumbukeni Bwana
ü  Daniel 8:25 Simama ushindane
KIROHO
Kusimama kiroho ni kuwa imara katika maswala ya kimungu ,uthabiti katika kile ulichodhamiria kukifanya.
Kusimama katika Bwana katika Imani.
Kusimama katika zamu yako
KIMWILI



C) ONDOKA  /  KUTOKA
Ni kuchukua hatua ya kuelekea au kutenda lengo kusudiwa.
Kuondoka kunambadilisha mtu na kunamfanya ajifunze mengi.
      N.B: Katika kuondoka :

o   Tunaondoka kiakili kwanza
o   Tunatumia miguu
Miguu inayopeleka injili imebarikiwa sana
Tembea uone
o   Kuna mwendo wa mwondoko
o   Kuna kuondoka kwa huzuni na kuondoka kwa furaha ni vema ukaondoka kwa furaha

NGUVU YA KUTOKA AU KUONDOKA
o   Mtumishi wa Mungu anapoondoka anakutana na Baraka tele huko aendako
  

Muombe Mungu akusimamishe.
ILI UWEZE KUONDOKA HAPO ULIPO UNATAKIWA KUFANYA MAMBO YAFUATAYO :
a)                         Usifurahie hali uliyo nayo ikatae hali hiyo,tamani kupanda viwango
b)                         Jisafishe nafsi yako kwa kuomba msamaha 1 korintho 5:7 
c)                         Tamani kuwa mtu wa viwango
d)                         Shirikiana na waliofanikiwa ,wenye hekima na waombe ushauri Mithali 13:20
e)                         Chukua hatua katika mipango uliyojiwekea
f)                          Linda sana moyo wako Mithali 4:23 ,Mathayo 7:21-23
g)                         Mngoje Bwana Zaburi 40:1
h)                         Tafakari Neno la Mungu  usiku na mchana Mithali 16:20
i)                           Ondoa mguu wako maovuni Mithali 4:27
j)                          Epuka kuwapa wengine heshima yako Mithali 5:9-10
k)                         Kuwa wewe kama wewe (Be yourself)
MAMBO YANAYOTUFANYA TUSHINDWE KUONDOKA TULIPO
  1. Dhambi  rumi 6:16 2 yohana 5:17
  2. Ujinga  yaani kukosa maarifa
  3. Mashaka ,masito na wasiwasi
  4. Moyo usiyokuwa mpya
  5. Imani haba
  6. Hofu
  7. Kutojitambua
  8. Kupenda kuwa tegemezi
  9. Kushindwa kujihatarisha
  10. Kutojiamini
FAIDA ZINAYOAMBATANA NA KUONDOKA/KUTOKA
  1. Unapoondoka unapata amani na furaha
  2. Unawekwa huru kweli kweli
  3. Mungu anakutetea
  4. Unalindwa na nguvu za Mungu kwa njia ya imani
  5. Unakuwa mshindi zaidi ya kushinda
  6. Unapona magonjwa yote
  7. Unatimiza kusudi la Mungu maishani mwako
MADHARA YA KUTOKUONDOKA MAHALI ULIPO

  1. Kupoteza uhai wao kama  Mke wa Lutu
  2. Kufanya mark time na kushindwa kubadilika
  3. Unaonewa na Ibilisi shetani
  4. Unakuwa Mtumwa wa dhambi
            MWALIMU JAMES SADY 0717 820 980

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni