MAJINA YA MUNGU
Katika maombi
ya vita ni vema tukatumia majina ya Mungu ya kivita ili aweze kutusaidia
kushinda maana Mungu hutenda kwa Jina lake Kutoka 3:13 6:3 Filipi 2:9-11
Hujibu maombi kulingana na unavyomuita .Mungu
anachukua nafasi ya Jina unalomuita na ndilo analotumia kutenda.Hivyo katika
maombi ya Vita tunahitaji kutumia majina ya Mungu yanayohusiana na Vita ili
Mungu aweze kutusaidia. Musa alipotaka
aelimishwe kwa undani kuhusu Mungu ili imani yake iimarike wakati wa kipindi
kisicho sahaulika sana cha maisha yake. Malaika,'Alitangaza Jina la BWANA: BWANA,BWANA Mungu,
Mwingi wa huruma, Mwenye fadhili, Si mwepesi wa hasira, Mwingi wa rehema na
kweli, Mwenye kuwaonea huruma watu elfu elfu, Mwenye kusamehe uovu na makosa na
dhambi; Wala si mwenye kumhesabia mtu mwovu kuwa hana hatia,’(Kut. 34:5-7). Musa aliambiwa
awaambie Jina la Mungu, ili kwamba hili liwasaidie kuwaletea kusudi la kuondoka
Misri na kuanza safari kuelekea nchi ya Ahadi (1Kor. 10:1) Nasi pia tunahitajika kuelewa mambo ya
msingi yahusuyo Jina la Mungu kabla ya kubatizwa na kuanza safari yetu ya
kuelekea Ufalme wa Mungu.
1. Jehovah Adonai => Bwana Mungu ,Mwenye
Enzi Yote (Mwanzo 15:2-8 , Malaki :6)
2.
Jehovah => Ajitegemeaye Kuwepo ,Mungu
wetu (Kut 6:2-8, Mdo 17:24-25)
3. Jehovah El – Shaddai =>Mungu Mwenyezi ,Mungu Mtoshelezi (Mwanzo
17:1, Kumb 8:4)
4. Jehovah El- Gibbor => Mungu ni Mkuu na Mwingi wa Nguvu ( Zab 147:5)
5.
Jehovah El-Elyon => Mungu Aliye Juu sana
(Mwa14:18, Dan
4:34)
6.
Jehovah El-Hai => Mungu Aliye
Hai/Anaishi ( Josh
3:10, 1sam17:26)
7. Jehovah El-Oheeka => Bwana Mungu Wako (Kutoka 20:2,5,7)
8. Jehovah El-Oheenu => Bwana Mungu Wetu (Zaburi
99:5,8,9)
9. Jehovah El-elohe-Israel =>Muumbaji Wa Milele (Mwanzo 33:20)
10. Jehovah
El-Olam => Bwana Mungu wa milele ,Bwana
Mungu Mwenyezi aliyekuwako na aliyeko na atakayekuja
(Ufu 4:8, Mwanzo 21:33)
11. Jehovah
El-Roi =>Mungu Aonaye Kila
Kitu
(Mith 15:3 )
12. Jehovah Hoseenu =>Bwana Aliyetuumba (Zaburi 95:6)
13. Jehovah
Jireh => Bwana
Atatupa",Mungu
Atupaye /Atoaye (Mwanzo
22:8, 13-14)
14. Jehovah
Maccaddeshem, Mekaddishkem,M’gaddishcem => Bwana niwatakasaye ninyi (Kut. 31:13)
15. Jehovah
Nissi =>"Bwana
Ni Ishara Yetu" ,”Bwana Ni Bendera(Beramu) Yangu”, Mungu ushindi wetu ( Kutoka 17:15 , 15:3)
16. Jehovah
Rapha,Iropheka => Mimi ndimi Bwana nikuponyaye (Kut
15:26 )
17. Jehovah Rohi => Bwana Ni Mchungaji Wangu ( Zab 23:1 )
18. Jehovah Sabaoth => Bwana Wa Majeshi (1
Samweli 1:3)
19. Jehovah Shalom => Bwana Ni Amani Yangu (Waamuzi 6:24,Amu 6:23-24 Isaya 9:6 )
20. Jehovah Shammah =>MIMI
NIKO AMBAYE NIKO ,MIMI NIKO ,Mungu yu pamoja nasi mahali pote na
wakati wowote
(Kut 3:14) (Ezekieli
48:35,Ebrania 13:5 )
21. Jehovah Tsidkemu (Sikenu,Tiskenu) => Bwana Ni Haki Yetu (Yeremia 23:6)
22. Jehovah
Yahweh => Bwana Mungu. (Mwanzo
2:4 )
23. Jehovah
Alfa and omega =>"Mungu
ni mwanzo na Mwisho” ( Ufunuo
1:8,21:6 22:13)
24. Jehovah Naheh => Bwana apigaye
(Ezekiel 7:9)
25. Jehovah’ori =>Bwana ni nuru yangu na wokovu
wangu ( Zaburi 27:1 )
26. Jehovah Sel’i => Bwana Ni Amani Yangu (Waamuzi 6: 24)
27. Jehovah Tsori =>Bwana Ni
Mwamba wangu na Mwokozi wangu ,Mungu Ngome yangu wakati wa Taabu (Zaburi
19:14 ) (Zaburi 37:39)
28. Jehovah Yasha => Bwana ni Mwokozi wako ( Isaya 49:26,60:16)
29. Jehovah
Chatsahi => Bwana ni ngome ya
uzima wangu (Zaburi 27:1)
30. Jehovah
izoz M’kaddesh => " Bwana atakasaye (sanctifier) ( 1 korintho 1:30)
31. Jehovah
Ez-Lami =>"Bwana ni nguvu
zangu na ngao yangu ” (Zaburi
28:7)
32. Jehovah Izoz Hakaboth => Bwana mwenye nguvu, hodari wa vita
- (Zaburi 24 :8 )
33. Jehova’Uzam=>Bwana Mwokozi
wako na Mkombozi wako ni mwenye enzi wa yakobo ( Isaya 49:26 )
34. Jehovah Kabothi => Bwana u ngao yangu pande
zote (Zaburi 3:3 )
35. Jehovah Kanna =>Bwana,Mungu mwenye wivu
(Kutoka
34:14)
36. Jehovah Keren-Yish’i => Bwana ni pembe ya wokovu wangu na
ngome yangu (Zaburi 18:2)
37. Jehovah
Machsi => Bwana Kimbilio langu (Zaburi
91:9)
38. Jehovah Magen => Bwana ni Ngao ya msaada wako ( Deut 33:29)
39. Jehovah
Ma’oz => Bwana ni ngome yangu
siku ya taabu (Yeremia
16:19)
40. Jehovah
Hamelech => " Bwana ni Mfalme (
Zaburi 98:6)
41. Jehovah
Melech’dam =>"Bwana ni
Mfalme wa milele na milele ” (Zaburi
10:16 )
42. Jehovah Mephalti => Bwana ni Mwokozi wangu (Zaburi 18:2)
43. Jehova Metsodhathi => Bwana ni jabali
langu,na boma langu langu (Zaburi 18:2)
44. Jehovah Misqabbi => Bwana ni ngome yangu (Zaburi 18:2)
45. Jehovah Adon Kal Ha’arets =>Bwana wa
dunia yote (Yoshua 3:13 )
46. Jehovah Bara => Mungu Muumba miisho ya dunia (Isaya 40:28)
47. Jehova Chezeq =>Bwana nguvu zangu (Zaburi
18:1 )
48. Jehovah chereb => Bwana ni upanga wa utukufu wako
( Kumbukumbu 33:29 )
49. Jehovah Eli => Bwana ni Mungu wangu
ninayemkimbilia (Zaburi 18:2)
50. Jehovah Gador Milchamah => Bwana mwenye nguvu, hodari wa vita (Zaburi 24:8 )
51. Jehovah
Ganan => Bwana Ni ngao yetu (Zaburi
89:18)
52. Jehovah Go’el => Bwana Mkombozi wako ( Isaya
49:26,60:16)
53. Jehovah
Hashopet => Bwana ni Mwamuzi (Waamuzi
11:27)
54. Jehovah
Hoshe’ah => " Bwana anaokoa ( Zaburi 20:9)
55. Jehovah’Immeku =>"Bwana yu pamoja nawe ” (Waamuzi
6:12)
56. Jehovah
El-Ohim => Mungu Muumbaji (Mwanzo
1:1 33:20 Kolosai 16-17)
Na MWALIMU JAMES SADY 0717 820 980
E-mail: “ jamesady9@gmail.com”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni