KUTAFUTA NA KUREJESHA
UWEPO WA MUNGU
- Uwepo wa Mungu ni nini?
=>Ni udhihirisho wa nguvu na
utendaji wa Mungu ndani na katikati ya watu.
Kinyume cha uwepo wa Mungu
ni uwepo wa shetani.
Upepo wa Mungu ni kama mtandao wa kijamii
(Network) .
Mungu ni moto ulao . Panapo uwepo wake kila
kitu kiovu kinalambwa .
Tofauti ya uwepo wa Mungu
ndani na katikati ya watu
NDANI
- Ndani ya mtu :matamanio ya mtu
binafsi kwa ajili ya maisha yake,vipawa na huduma yake
KATIKATI
- Uwepo wa Bwana unatakiwa
kuwaunganisha wacha Mungu wote kwa pamoja na umoja ndiyo maana Yesu
aliwaombea pamoja kwa umoja.Yohana 17 (Wana kanisa la Bwana)
- Katikati yenu nitatembea
- Umuhimu wa uwepo wa Mungu
- Hakiharibiki kitu
- Hapunjwi mtu
- Watu wanainuliwa
- Watu wanabadilika mwilini na rohoni
- Udhihisho wa ishara na maajabu :
uponyaji,ufufuo...
- Watu wanafunguliwa
- Uwepo wa Mungu nyakati za Agano la kale na Agano jipya.
a) Agano la kale
Nguvu ya madhabahu
- Moto wa madhabahu
b) Agano jipya
- Uwepo wa Mungu ndani ya Yesu Kristo mwenyewe.
Ulianza kudhihirika alipobatizwa na Yohana Mbatizaji.
Kilichotokea katika tukio la kubatizwa kwake:
-Sauti ya Mungu ilisikika
-Roho wa Mungu alishuka juu ya Yesu(Ujio wa Roho Mtakatifu )
Baada ya
kubatizwa na uwepo wa Bwana kushuka kupitia haya mambo mawili,Yesu aliendelea
kuutafuta na kuutunza mpaka pale yule mwanamke aliyekuwa anatokwa damu
alipomgusa na uwepo wa Mungu ukapungua .
Yesu alizoea
kwenda mlimani kuuchochea uwepo huo kwa njia ya maombi.
MANENO SABA ALIYOYASEMA
YESU MSALABANI
a)Baba uwasamehe kwa maana
hawajui walitendalo Luka 23:41
b)Leo utakuwa pamoja nawe
peponi Luka 23:43-44
c)Mwanamke tazama mwana wako,tazama mama yakoYohana 19:26-27
d)Mungu wangu Mungu wangu
mbona umeniacha?(Eloi Eloi lama sabaktani Mathayo 27:46 2 korintho 5:21)
e)Nina kiu Yohane 19:28
f)Imekwisha Yohane 19:30
g)Baba Mikononi mwako mwako naiweka Roho yangu
Luka 23:46
- Uwepo wa Mungu katika agano jipya ulianza kudhihirika rasmi Siku
ya pentekoste aliposhuka Roho
Mtakatifu na uliendelea kuonekana
Katika ushirika wa wana wa
Mungu.
- Mambo ambayo uwepo wa Mungu unaweza kufanya
Uwepo wa Mungu unaweza:
·
Kuja
·
Kupotea
·
Kupungua
·
Kutembea
·
Kuondoka(kuachwa
na Mungu kwa siri)
- Vitu vinavyovuta uwepo na vinavyoondoa uwepo wa Mungu (Ikabodi)
Kanuni za kuuvuta uwepo wa Mungu:
a)Ibada katika roho (sadaka)
b) Kumuita
Mungu (Maombi,sala,dua)
mfano : Yesu alimuita Baba “Eloi Eloi Lama sabaktani”
Eloi ni maombi lakini tena ni kilio
- Dalili za uwepo wa Mungu mahali.
Mfano : Siku za pentecoste
Penye uwepo wa Mungu
pana mambo yafuatayo:
Ishara na maajabu hutendeka.
Faida za ishara na maajabu
a)isahara na maajabu husababisha mshangao kwa wasiyoamini Matendo 2:7 na
3:10
b)ishara na maajabu husababisha watu kuingiwa na hofu ya Mungu Matendo 2:43
c)ishara na maajabu husababisha watu kumtukuza Mungu Mtendo 4:21
d)ishara na maajabu husababisha furaha kubwa Matendo 8:8
e) ishara na maajabu huvuta imani iokowayo Matendo 9:42 1 Wakorintho 2:4-5
Makusudi ya ishara na maajabu katika agano jipya
a)kuhakikisha uungu wa Kristo na kuwafanya watu waamini.Matendo 2:22
Ebrania 2:4
b)kuwavuta watu wasikilize injili
c)kama ushahidi kwamba Kristo yu hai na ni Bwana wa kanisa .
d)kuthibitisha Neno lililohubiriwa Matendo
4:29-30 Matendo 14:3 Rumi 15:19 Ebrania 2:3-4
e)kutambulisha waumini wa dini ya kweli 2
Korintho 12:12 Marko 16:15-18
f)kukutana na mahitaji ya mwanadamu
g)kuendeleza ufalme wa Mungu duniani Matendo
5:12-14 Matendo 8:5-13
- Dalili za kuondokewa na uwepo wa Mungu mahali au ndani ya maisha ya mtu.
Kanisa lenye
kujaa uwepo wa Mungu
|
Kanisa lisilo
na uwepo wa Mungu
|
Umoja wa
washirika
Ishara na
maajabu halali hudhihirika
Watu wanakuwa
kiroho
Waumini
wanadhihirisha upendo wa dhati baina ya yao kwa wao
Viongozi
hupatana katika mambo yote
|
Watu
wanagawanyika
Migogoro
Ushindani
Kubaguwana
Ushabiki wa
kiroho
Kudumaa na
kusinyaa kiroho
Kupoteza
Watu
hawabadiliki
|
- Kudumisha na kulinda uwepo wa Mungu.
Mifano ya jinsi uwepo wa Bwana ulivyodumishwa
katika agano la kale na agano jipya
a)Agano la kale
·
Ili
kudumisha uwepo wa Mungu katika Nyakati za manabii ilitegemea uwepo wa sanduku
la agano na huduma takatifu za madhabahu
Madhabahu yalibeba mambo
yafuatayo:
·
Kuhani mkuu wa madhabahu
·
Sadaka juu ya madhabahu ambapo kafara ya
damu ilikuwa inatolewa
·
Biblia inasema kwamba Moto wa madhabahu
usizimike na wao walikuwa wanawasha kinara cha taa kila wakati masaa yote bila kukoma kama alama ya
kutunza uwepo wa Mungu.
b)Agano jipya
- Ili kudumisha uwepo wa Mungu katika
Nyakati za mitume ilitegemea misingi minne iliyojengwa katika neno”kudumu” katika :
- Fundisho
- Kusali
- Ushirika
- Kumega mkate
Matokeo ya mambo haya yalileta
mlipuko wa uwepo wa Mungu uliyosababisha ishara
na maajabu kutendeka kwa kiwango kikubwa katika mikono ya mitume.
Kitu kilichosababisha HOFU ya Mungu
katika watu.
Uwepo wa Mungu unadumishwa kwa :
b) Kuutamani na kuutafuta
Mithali 18:17
“Mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kuwa yeye
yupo na kwamba huwapa dhawabu wale wamtafutao” ( Ebr 11:6).
Unatafutwa kwa njia ya Toba kamili.
·
Mungu
alipotaka kuzungumza na wana wa Israel kwenye mlima Sinai aliomba wajitakase
kwanza
Ni vema tumuombe Mungu :
·
Kukutana
na Bwana
·
Kukaa
uweponi mwa Mungu
·
Kufunikwa
na uwepo wa Mungu
·
Kutembea
katika uwepo wa Bwana
·
Uwepo
wa Mungu mahali tulipo
Uwepo wa Mungu unadumishwa kwa:
·
Kuishi
maisha matakatifu
·
Kutii
sheria ya Mungu
·
Kutembea
na kuongozwa na Roho Mtakatifu
- Uwepo wa Mungu katika maeneo tofauti tofauti
Katika ardhi,anga ,huduma ,mtu
kiutendaji.
Uwepo wa Mungu waweza kuja
kwa njia ya kutoa kibali katika viumbe :
a) Mazingira : (laws and rules )
ndege-hewa
samaki –maji
mimea –ardhi
mwanadamu –Mungu
Jengo : Ofisini,nyumbani ,kanisani,
Eneo/Mahali
fulani : shamba , maeneo tofauti tofauti ya Nchi,katika barabara fulani
Mifano :
1.Musa na Yoshua waliambiwa wavue
viato vyao kwa kuwa mahali pale palikuwa ni patakatifu
2.Nchi ya israeli yote
imebarikiwa kuwa nchi yenye rutuba kila mahali ukipanda
mbegu yoyote inachipuka na kukomaa.
b) Viungo vya mwili :
Mikono iliyobarikiwa inaponya
Miguu iliyobarikiwa ikikanyaga
inatawala
c)Mavazi
:pindo la Yesu ,Leso aliyoitumia Paulo
d) Vitu
mbalimbali: udongo aliyoutumia yesu kumponya Bartimayo
NA MWALIMU JAMES SADY 0717 820
980
E-MAIL: jamesady9@gmail.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni