Jumamosi, 24 Septemba 2016

SABABU ZINAZOWEZA KUSABABISHA MAOMBI YAKO YASIJIBIWE


Ndugu katika Krito , Bwana Yesu asifiwe,
Wakristo wengi wanaomba lakini hawapokei majibu ya mahitaji yao kutokana na kutokufahamu sababu mbalimbali zinzazoweza kuwa sababisho la Mungu kutokujibu maombi yao. Wengi wanachoka kuomba baada ya kuona wanacheleweshewa majibu ya mahitaji yao lakini wanasahau kwamba zipo kanuni wangepaswa kuzifuata ili kuweza kupata majibu ya mahitaji yao kirahisi.
Maandiko yanasema katika kitabu cha Mathayo 7:7 Ombeni nanyi mtapewa ,tafuteni nanyi mtaona ,bisheni nanyi mtafunguliwa” Maneno haya  hayafanyi kazi kwa kila mtu ili mradi tu ameomba bali yanafanya kazi kwa watu maalumu wanaofuata kanuni za kiungu na kutendea kazi Neno la Mungu.
Hao  wanaoomba na kupewa ni Wana wa Mungu walio katika zizi la Kondoo wa Mungu si wale walio nje ya zizi la Kondoo wa Mungu au sio wale wasiofuta kanuni ,miiko na sheria za kiroho.Si rahisi mzazi akamsikiliza motto mkaidi,asiye mtiifu kwake ,anayesufuata mambo yake binafsi kwa maana anakuwa tayari kama mwana mpotevu.Yampasa huyo mtoto kwanza arudi nyumbani kwa mzazi wake ndiposa Mzazi ataweza kumkaribisha kwa furaha ,kumhudumia na kumsaidia katika mahitaji yake yote ya kiroho na kimwili.Itakuwa rahisi kumsikiliza mtoto wake watakapokuwa wapo pamoja.  
Biblia inasema kwamba Maombi ya Mwenye dhambi ni kelele mbele za Mungu na hivyo kuna haja ya kuwa msafi kwanza kabla ya kuomba ili upate majibu ya mahitaji yako kirahisi .Hiyo itatokea mara baada ya kurudi nyumbani mwa Mungu,ukatubu dhambi zako na kuanza kufuata kanuni za Kimungu.
Tena maneno ya Mungu yanasema hivi  Isaya 43:26 “Unikumbushe na tuhojiane ,eleza mambo yako upate kupewa haki yako” kwa maana kwamba zipo haki za mwana wa Mungu na ili kuzipata haki hizo inampasa amkumbushe Mungu na wahojiane ili baada ya Mungu kujiridhisha na Halie yake ya kiroho na namna anavyomuomba ipasavyo basi na ampe haki zake .
Biblia pia inasema kwamba tumletee Mungu hoja zenye nguvu Isaya 41:21 “kwa maana kwamba endapo tutamuomba Mungu bila kutoa hoja zenye nguvu yaani zenye mashiko na zenye mantiki nzuri hatutoweza kupokea kile tunachokiomba
Mungu ni Mungu wa Kanuni ,kabla ya kumjibu muombaji lazima atataka kujiridhisha kutokana na kile anachokiomba kuangalia kama kinaendana na Kanuni za kimungu za kupokea Majibu ya mahitaji.
Kabla ya kujibu muombaji Mungu anaangalia mambo yafuatayo:
  1. Hali ya kiroho ya muombaji
·         Yaani ukoje katika hali yako ya uhusiano wako na Mungu?
·         Umejiandaje kupokea majibu ya mahitaji yako?
·         Ufahamu wako una uwezo kiasi wa kustahimili nguvu ya majibu ya mahitaji yako?
·         Je hoja yako ina nguvu mbele za Mungu?
·         Una mzigo kiasi gani ndani yako wa kazi ya Mungu?
  1. Namna anavyoomba
·         Unaombaje ?
·         Unaomba kwa kusudi/lengo gani ?
·         Kwa nini unaomba kitu hicho
·         Jambo unaloliombea linasaidia vipi kupanua ufalme wa Mungu?
·         Nia au msukumo wako wa kuomba kitu hicho  ni nini?
Hivyo basi tuna kila sababu ya kujipima katika kuzichunguza sababu zinazoweza kusabababisha tukakosa kupata majibu ya mahitaji yetu.
Kuna makundi makuu manne ya sababu zinazofanya maombi ya wanadamu yasijibiwe na Mungu:
·      Dhambi za kiroho (Spiritual sins) – Mashaka ,Unafiki, Kiburi,mambo ya upuuzi,mzaha,kejeli  etc
·      Ukosefu wa uhusiano (Poor relationships) - ,kutokusamehe,ushenzi,fidhuli, uovu, Hasira, ghadhabu,matengano.
·      Dhambi  - mambo yote yanayohusiana na kutenda uovu(1 Kor 6:9,10)
·      Kuomba vibaya  -kukosa msimamo,Kukata tamaa, kutokufunga,kutokutumi Jina la Yesu etc.
Sababu hizo ni pamoja na :
1.      Kutokuomba kwa Jina la Yesu  Kristo Yohana 2:17-26  14:13-14 (Marko 16:17-18).
2.      Kutokutubu dhambi au kutokuomba Msamaha Isaya 59:1-2
3.      Kuwa na mashaka na maneno uliyoyasema ulipokuwa unaomba  marko 11:23
4.      Hali ya Kusitasita moyoni au Kuwa na mashaka na Mungu Yakobo 1:5-8 
5.      Kutokuamini Yesu Kristo Yohana 16:26-27
6.      Kutokuomba Mungu Yakobo 4:2
7.      Kuomba kitu unachotaka kitumie kukidhi tamaa yako yaani kuomba vibaya Yakobo 4:3
·         Tunapaswa kuomba mambo yanayoendana na mapenzi ya Mungu au yanayoleta utukufu wa Mungu .
8.      Kukosa maneno ya Mungu ya kutosha ndani ya moyo Yohana 15:7
9.      Kutokuwa mtendaji wa Neno la Kristo au kutenda mabaya 1 Petro 3:12
10.  Kukosa kukesha 1 Petro 4:7
11.  Kuhukumiwa na moyo binafsi 1 Yohana 3:21-23
12.  Unafiki katika sala  Mathayo 6:5,6
·         Kuomba ili uonwe na watu
13.  Kupayuka-payuka katika sala Mathayo 6:7
14.  Kukosa umoja miongoni mwa viongozi wa kikristo ,kutokupatana Mathayo 18:19
15.  Kukosa kifungo cha roho Marko 9:29
16.  Kutokusamehe Marko 11:25-26
·         Kabla ya kuomba unatakiwa kusamehe waliokukosea kwanza.
17.  Kukosa subira na kukata tamaa Luka 18:1-8
18.  Kiburi  Luka 18:11-12
19.  Hasira /ghadhabu na majadiliano 1 Timotheo 2:8
20.  Mazungumzo mabaya   1 korintho 15:33
Zaburi 66:18 mawazo mabaya
21.  Kutokuamini Ahadi za Mungu (imani haba)
22.  Kuendeleza uovu 2 Timotheo 2:19
23.  Tamaa mbaya 2 Timotheo 2:22
24.  Ugomvi 2 Timotheo 2:23 1 Timotheo 3:3
25.  Kushiriki dhambi za wengine 1 Timotheo 5:22
26.  Kushindwa kutunza walio wako 1 Timotheo 5:8
27.  Kushindwa kuzuia nafsi 1 Timotheo 5:6
28.  Kujaa Lawama 1 Timotheo 5:7
29.  Kutokuomba sawasawa na mapenzi ya Mungu 1 Yohana 5:14-15
30.  Kutokaa ndani ya Yesu Yohana 15:7
31.  Kuwa na imani isiyo na matendo Yakobo 2:17
32.  Kutosikia kilio cha wahitaji Methali 21:13
33.  Kutoshukuru Mungu (shukrani)Filipi 4:4-12
34.  Kutokaa kwa amani na mke wako
1 PETRO 3:7 [‘Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili; na kumpa mke heshima, kama chombo kisicho na nguvu; na kama warithi pamoja wa neema ya uzima, kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe’].


MWALIMU JAMES SADY 0717 820 980

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni