Matendo
ya Mitume 12: 1-19, zingatia sana mstari wa 7 unaosema; "...Ondoka upesi,
Minyororo yake ikamwanguka mikononi"
ISAYA 60:1
"Ondoka uangaze; kwa kuwa nuru yako imekuja,
Na utukufu wa Bwana umekuzukia."
"Ondoka uangaze; kwa kuwa nuru yako imekuja,
Na utukufu wa Bwana umekuzukia."
Anaposema, ONDOKA anamaanisha Utoke hapo ulipo pia
Uinuke kutoka hapo ulipo maana ni mahali pa mateso yako, mahali pa huzuni yako
na ni mahali palipokuchelewesha sana hivyo:
- Ondoka kwenye kuumwa umwa na uangaze ukiwa na uzima ndani yako.
- Ondoka kwenye kujikataa maana kulisababisha ukataliwe lakini leo ondoka hapo na Mataifa yatakujilia maana NURU YA BWANA IPO JUU YAKO (ISAYA 60:3)
*Magonjwa
* Umasikini
* kufeli
* kushindwa hakupo tena juu yako maana hiki ni kipindi chako cha KUINUKA NA KUANGAZA MWANA WA MUNGU.
- Ondoka kwenye kuumwa umwa na uangaze ukiwa na uzima ndani yako.
- Ondoka kwenye kujikataa maana kulisababisha ukataliwe lakini leo ondoka hapo na Mataifa yatakujilia maana NURU YA BWANA IPO JUU YAKO (ISAYA 60:3)
*Magonjwa
* Umasikini
* kufeli
* kushindwa hakupo tena juu yako maana hiki ni kipindi chako cha KUINUKA NA KUANGAZA MWANA WA MUNGU.
ONDOKA KATIKA TABIA ZA
KWANZA
Isaya 60:1-2
"Ondoka, uangaze; kwa kuwa nuru yako imekuja, Na utukufu wa Bwana
umekuzukia.Maana, tazama, giza litaifunika dunia, Na giza kuu litazifunika
kabila za watu; Bali Bwana atakuzukia wewe, Na utukufu wake utaonekana juu
yako."
Ukiokoka jambo la kwanza amua kubadilika na
uamuzi wa kubadilika unao wewe mwenyewe. Mtu akikuangalia akilinganisha maisha
yako kabla ya kuokoka na baada ya kuokoka aone umebadilika. Katika kuondoka
ndipo tunakutana na Utukufu wa Mungu, lakini ukiwa katika tabia za kwanza
hutaona Utukufu wa Mungu. Utasikia wengine
wakisimulia matendo ya MUNGU lakini kwako hutayaona.
Hapo kwanza ulikuwa mtu wa kawaida lakini leo
kuna watu wakipata shida wanakutafuta ni kwasababu umeamua kuondoka.
Ukiona watu wanakusifia kwa mambo ya jana
inamaana huna jipya leo, wokovu wetu ni sasa siyo jana, usijivune kwa jambo la
jana bali jivune kwa jambo zuri unalofanya leo. Ni vizuri kuishi kwa tahadhari
ili NURU yako isitiwe giza.
Tunatakiwa tusiishi kama watu wasio na matumaini bali tuishi kama wasafiri, wakati wote wana wa MUNGU tunatakiwa kuwa na muda wa ziada wa kujiandaa kwa safari.
Ugomvi wetu na MUNGU uko kwenye tabia zetu,
hazitaki kubadilika na kuhama katika tabia za kale, lakini kuanzia leo
hatutazikumbuka tena tabia za kale na tukizikumbuka ni ili kutubu na kutorudia
tena. Mungu hajakuokoa ili ukae kanisani uonekane ni Mkristo hapana, amekuokoa
kwa kusudi na mpango wake. Jichunguze ulipo ni sawa na hilo kusudi?
Ukiona mwenzako amefanikiwa na kuchanua, MUNGU
anambariki au anafanya vizuri katika utumishi wake na wewe unamzuia au roho
inaumia ujue wewe na pepo hamna tofauti maana unapingana na MUNGU, ukijua wewe
ni mtu wa aina hiyo rudi umwambie MUNGU sitaki kuwa kama pepo nisamehe na
unibadilishe.
Wana wa mungu ukiona mwenzako amefanikiwa nenda kamuulize, mwenzangu unatumia mbinu gani? Sio unaanza kumwekea kinyongo. Haupo ili kumsaidie shetani bali unatakiwa kumsaidia MUNGU maana sisi ni MIUNGU.
Wana wa mungu ukiona mwenzako amefanikiwa nenda kamuulize, mwenzangu unatumia mbinu gani? Sio unaanza kumwekea kinyongo. Haupo ili kumsaidie shetani bali unatakiwa kumsaidia MUNGU maana sisi ni MIUNGU.
1.
Mungu alimwambia Ibrahimu atoke katika Nchi ya baba yake
2.
Lutu na jamaa yake walikaa Kanaani
pamoja na Ibrahimu na baada ya muda waliachana wakagawana ardhi Lutu akachagua
Wilaya ya Yordani akahamia huko na jamaa yake na wanyama hatimaye wakakaa
katika mji wa sodoma ..watu wa sodoma walikuwa wabaya sana ,Lutu alisumbuliwa
maana alikuwa mtu mzuri.Hata Mungu alisumbuliwa. Mwishowe Mungu alituma malaika
wawili wakamwonye lutu kwamba Mungu ataharibu sodoma na gomora mji wa karibu
maana ni miji mibaya.malaika wakamwendea Lutu wakamwambia “Fanya haraka ,chukua
mke wako na binti zako wawili MWONDOKE huku! Malaika mmoja
alisema “Kimbieni kwenye milima msiuawe”Lutu na binti zake WAKATOKA
sodoma lakini mke wa Lutu hakutii .walipokwisha kutembea mwendo Fulani kutoka
sodoma ,mke alisimama akatazama nyuma akawa nguzo ya chumvi.
Mwa 13:5-13 18:20-33 19:1-29 Luka 17 :28-32 2 Petro 2:6-8
3.
Yohana 5:7 Sina mtu wa kunitia birikani
Luka 5: 24-26 Ondoka
,jitwike kitanda chako,ukaende zako
nyumbani kwako.
Yohana 11:39 liondoeni jiwe.
Mathayo 23: 35 Mwanamke aliyetokwa na damu. Mwanamke huyu aliondoka
kwenye taabu yake (Magonjwa )
USHAURI
o Usifurahie kukaa mahali
ulipo kwa muda mrefu maana siyo mpango
wa Mungu udumae usitoke hapo ulipo
o Kamwe usiridhike na
hali uliyonayo .
o Lazima cheo chako na
hadhi yao viendane.
Kazini Mungu anahitaji upande viwango
Katika huduma Mungu anapenda huduma yako iongezeke zaidi
Katika biashara Mungu anahitaji uongeze mtaji na
upate maendeleo ya ziada
Mungu :
o
Ni Mungu wa maendeleo
o
Ni Mungu wa mazao
o
Ni Mungu wa maongezeko
o
Ni Mungu Mtawala
o
Ni Mungu wa viwango
o
Ni Mungu wa mabadiliko
o
Ni Mungu wa tofauti
Mungu anatumia alama ya :
a)
kujumlisha (+) na
b)
kuzidisha (X)
c)
kugawa ( : ) Luka 5:7
Aliye na joho mbili
ampe na mwingine Mathayo 10 :
Hali kadhalika anatutaka na sisi pia tuwe kama yeye
alivyo .
o
TUENDELEE
o
TUZAE (Anataka tumzalie matunda ya
kiroho na ya kimwili)Mwanzo 1:28
o
TUONGEZEKE (anataka tuongezeke katika maeneo yote ya maisha yetu) Mwanzo
1:28
o
TUIJAZE NCHI Mwanzo 1:28
o
TUTAWALE tusitawaliwe
o
TUWE NA VIWANGO
o
TUBADILIKE
o TUWE WA TOFAUTI
Mpango wa Shetani ni
kutaka sisi tukwame ,tusisonge mbele ,tudumae tusiendelee wala kupata mafanikio
hata kidogo . Kazi yake ni kuiba ,kuharibu na kubomoa Yohana 10:10
Mungu anataka tutoke/
katika :
Aina za mikwamo:
a)
Mkwamo wa kimwili
b)
Mkwamo wa kiroho
MKWAMO WA KIROHO
1)
Imani haba na potovu( Uchanga wa kiroho )
2)
Tabia mbaya
3)
Upofu wa kiroho (bartimayo)
Efeso 1:6 Macho ya
mioyo yatiwe nuru mpate kujua kusudi la
Mwito wenu katika Kristo Yesu.
MKWAMO KIMWILI
1)
Magonjwa
2)
Ufukara
3)
Ujinga
Hatua za kuondoka mahali ulipo:
1.
KWANZA
UNAINUKA
2.
PILI
UNASIMAMA
3.
TATU
UNAONDOKA
A) INUKA
Isaya 62:1 Inuka uangaze maana nuru yako imekuja.
…………..Inueni
vichwa vyenu enyi malango
Huku kuinuka kunatokana na maamuzi uliyonayo ya
kuchoka hali uliyonayo kwanza na ukaamua kuiacha
Kuinuka ni kufanya mkaguo wa maisha yako ,unafanya
tathmini ya maisha yako
Kuinuka ni kugundua tatizo na kusudi la kuumbwa
kwako.
Mifano :
a)
Mwana
mpotevu akawaza moyoni mwake .
b)
Mwanamke aliyekuwa anatoka damu.
KIU ,TAMAA,SHAUKU
Kabla ya kuinuka unahitaji kwanza shauku ,hamu ,kiu
(desire )ya kuwa vile unavyotaka kuwa .
“Huwezi kuwa usivyotamani kuwa”
Ila waweza kutamani. Kutamani kuwa katika viwango
vingine vya utumishi na imani
KUFUNGWA
KWA AKILI
o Watoto waliozaliwa
kwenye mlima wakakulia huko huko walipopelekwa barabarani na mjini walishindwa
kuelewa.
o Wengine wamefungwa na
mila zao na tamaduni.(uchawi ,ulozi)
o Wengine wana maono ya
kanisa moja tu mapokeo ya kanisa na itikadi za dini yake.
o Wengine wana maono ya
mkoa moja au wilaya .
o Wengine wanaona familia
zao tu hawajali jamii Biblia inasema
“Enendeni ulimwenguni mwote”
KUNA WATU WAMERIDHIKA NA HALI ZAO HAWATAKI KUONDOKA
WALIPO
a)
Mlemavu moja alikuwa ombaomba ,alizoea upata hella nyingi.siku moja akaja
mtumishi wa Mungu kumuombea uponyaji asiwe mlemavu yeye akakataa kwamba hawezi
kukubali kuombewa kwa sababu anaogopa atakavyoishi baadaye.
VITU
VINAVYOINUA MTU
b)
Kuishi maisha ya maombi
c)
Kuthubutu :kuchukua hatua ya kuanza kitu Fulani la Maendeleo
o Mwanamke aliyekuwa
birikani alishindwa kuthubutu kujaribu kuingia birikani.
d)
Kuanza mawazo ya biashara na kuiendeleza
Mtu anaweza kuajiriwa mahali lakini anazidi
kulalamikia bosi badala ya kuchukua hatua ya kutafuta kazi sehemu nyingine.
B) SIMAMA
Isaya
3:13
Bwana asimama ili atete
Isaya
40:8 Shauri langu litasimama
Kusimama ni tabia
ya Mungu maana halali wala
hasinzii .
ü Nahumu 2:8 Simameni ,simameni ,simameni.
ü Mika 6:1 Simama
ujitetee.
ü Mika 7:8 Niangukapo
nitasimama tena.
ü Habakuki 2:1 Nitasimama
katika zamu yangu
ü Efeso 6:13 Simameni
hali mmejifunga kweli viunoni
ü Yohana 8:44 Simama
katika kweli
ü Ezekiel 2:1 Mwanadamu
simama kwa miguu
ü Ezekiel 22:30 Simama
mahali palipobomoka
ü Yeremia 46:4 Simameni
na chapeo zenu
ü Yeremia 51:50 Msimame
mkumbukeni Bwana
ü Daniel 8:25 Simama
ushindane
KIROHO
Kusimama kiroho ni kuwa imara katika maswala ya
kimungu ,uthabiti katika kile ulichodhamiria kukifanya.
Kusimama katika Bwana katika Imani.
Kusimama katika zamu yako
KIMWILI
C) ONDOKA
/ KUTOKA
Ni kuchukua hatua ya kuelekea au kutenda
lengo kusudiwa.
Kuondoka kunambadilisha mtu na kunamfanya ajifunze
mengi.
N.B:
Katika kuondoka :
o Tunaondoka kiakili
kwanza
o Tunatumia miguu
Miguu inayopeleka
injili imebarikiwa sana
Tembea uone
o Kuna mwendo wa mwondoko
o Kuna kuondoka kwa
huzuni na kuondoka kwa furaha ni vema ukaondoka kwa furaha
NGUVU YA KUTOKA AU KUONDOKA
o Mtumishi wa Mungu
anapoondoka anakutana na Baraka tele huko aendako
Muombe Mungu akusimamishe.
ILI UWEZE KUONDOKA HAPO ULIPO UNATAKIWA KUFANYA
MAMBO YAFUATAYO :
a)
Usifurahie hali uliyo nayo ikatae hali hiyo,tamani kupanda viwango
b)
Jisafishe nafsi yako kwa kuomba msamaha 1 korintho 5:7
c)
Tamani kuwa mtu wa viwango
d)
Shirikiana na waliofanikiwa ,wenye hekima na waombe ushauri Mithali 13:20
e)
Chukua hatua katika mipango uliyojiwekea
f)
Linda sana moyo wako Mithali 4:23 ,Mathayo 7:21-23
g)
Mngoje Bwana Zaburi 40:1
h)
Tafakari Neno la Mungu usiku na
mchana Mithali 16:20
i)
Ondoa mguu wako maovuni Mithali 4:27
j)
Epuka kuwapa wengine heshima yako Mithali 5:9-10
k)
Kuwa wewe kama wewe (Be yourself)
MAMBO
YANAYOTUFANYA TUSHINDWE KUONDOKA TULIPO
- Dhambi rumi 6:16 2 yohana 5:17
- Ujinga yaani kukosa maarifa
- Mashaka
,masito na wasiwasi
- Moyo
usiyokuwa mpya
- Imani
haba
- Hofu
- Kutojitambua
- Kupenda
kuwa tegemezi
- Kushindwa
kujihatarisha
- Kutojiamini
FAIDA
ZINAYOAMBATANA NA KUONDOKA/KUTOKA
- Unapoondoka
unapata amani na furaha
- Unawekwa
huru kweli kweli
- Mungu
anakutetea
- Unalindwa
na nguvu za Mungu kwa njia ya imani
- Unakuwa
mshindi zaidi ya kushinda
- Unapona
magonjwa yote
- Unatimiza
kusudi la Mungu maishani mwako
MADHARA
YA KUTOKUONDOKA MAHALI ULIPO
- Kupoteza
uhai wao kama Mke wa Lutu
- Kufanya
mark time na kushindwa kubadilika
- Unaonewa
na Ibilisi shetani
- Unakuwa
Mtumwa wa dhambi
MWALIMU JAMES SADY 0717 820 980
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni